HABARI ZA TOWN: michezo

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...
Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Simba Wataka Kufanya Maandamano ya Amani, Wamechoshwa na TFF


KUFUATIA sakata la kamati ya katiba, hadhi na wachezaji kuliweka tena mezani suala la Klabu ya Simba kupewa pointi 3 dhidi ya Kagera baada ya kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, wekundu hao wa Msimbazi wametuma barua kwa Kamanda kwa kanda maalum Mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro kuomba maandamano ya amani. 

Maandamano hayo amb kwa mujibu wa barua hiyo ya leo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne kuanzia majira ya saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana yakianzia Makao Makuu ya klabu hiyo kuelekea  Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dhumuni kuu la barua hiyo ni kupinga namna Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufanya vitendo na maamuzi ya uonevu kwa Klabu ya Simba huku malalamiko mengi ya msingi wanayopeleka maombi yakiwa hayasikilizwi kwa wakati. 

Mbali na hilo ni pamoja na leo, Shirikisho hilo kuamua kumpeleka Msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili ikiwa wanaonyesha nia ya kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asioongelee uonevu unaofanywa dhidi yao. 

Barua ya kuomba maandamano hayo ya amani imendikwa na Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva na kutuma nakala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na maandamanio hayo yatapitia katika barabara za Msimbazi, Nyerere na Chang'ombe. 

BARCA,DORTMUND WERE THROWN OUT OF THE UEFA CHAMPIONS LEAGUE!!

BARCELONA na Borussia Dortmund zimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kupenya kwenye mechi za robo fainali ilizocheza dhidi ya Juventus na AS Monaco.

Barcelona iliyocheza na Juventus ilitupwa nje kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya jana Jumatano huko Nou Camp, huku Borussia Dortmund wao wakitupwa nje kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya kuchapwa 3-1 usiku huo wa jana. Katika mechi za kwanza za hatua hiyo ya robo fainali, Barca ilichapwa 3-0 Turin, Italia wiki iliyopita wakati Dortmund wao walichapwa 3-2 kwaUjerumani.BARCELONA na Borussia Dortmund zimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kupenya kwenye mechi za robo fainali ilizocheza dhidi ya Juventus na AS Monaco.

WACHEZAJI 2 MUHIMU MOURINHO ANAOWATAKA KUUNGANA NA ZLATAN! MAN UTD

JOSE MOURINHO anashawishika sana kumtaka  Romelu Lukaku na Antoine Griezmann ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na wachezaji hao kuungana  Zlatan Ibrahimovic  Manchester United.
The Old Trafford boss ametenga kiasi kikubwa cha pesa (Mtonyo) wa  £160million kwaajili ya kuimarisha kikosi chake na pia kumuacha kipenzi cha Manchester united Wayne Rooney ambae anajiandaa kuondoka Klabuni hapo..
Mourinho pia anataka kumfanya Ibra kuwa godfather mpya wa  Old Trafford  kwa kumuongezea mkataba mpya wa kumfanya mswedeni huyo kubaki OT kwa mwaka mwingine tena wenye thamani ya  £10m.
The Special One kesho anaingia kwenye mchezo mgumu na wa muhimu watakapokutana na Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani OT ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya timu yake kurudi kwenye Champions League..
Wachezaji ambao Mourinho anawafukuzia kwa muda mrefu bila kukata tama ni Antonie Griezmann wa Athletico Madrid, Dili la mchezaji huyo litafanikiwa zaidi kama Manchester united wakifanikiwa  kumaliza Top 4 kwenye Epl na kwenda Champions League.
.

Pia mchezaji mwingine ambae Jose anamfukuzia ni Romelo lukaku ambae alimpeleka West Brom kwa mkopo na baadae  kwenda Everton wakati anaifundisha Chelsea kabla ya kutua kwa mashetani wekundu..
Swali ni moja tu  kwako mdau wa Perfect255 Je, Jose Mourinho atafanikiwa zaidi kwenye kikosi chake akishawaongeza hawa wachezaji anaowataka???

THOMAS ULIMWENGU HATARINI KUSOTA BENCHI KWA MAJUMA 12

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden, Thomas Ulimwengu atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu akiuguza jeraha la goti.
Ulimwengu aliyejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwezi Januari alipata majeraha hayo mwezi uliopita hali iliyopelekea akose mechi mbili za kirafiki za Stars dhidi ya Botswana na Burundi licha ya hapo awali kuitwa na kocha Jackson Mayanja.
Katika Interview wiki hii na Times FM kupitia kipindi cha Wizara Ya Michezo imezungumza na mshambuliaji huyo kutoka nchini Sweden, ambapo alisema ameelezwa na daktari kuwa atalazimika kukaa nje kwa majuma 12 ili aweze kurejea katika hali yake.
“Niliumia wiki kadhaa zilizopita na ni kama vile nilipona nikaanza mazoezi ndipo nikajitonesha, sasa nimetoka kwa daktari hapa muda huu ameniambia nipumzike kwa miezi mitatu ndipo nitakuwa fit,”alisema Ulimwengu.
Tayari Ulimwengu ambaye alishaanza kuonyesha makeke mazoezini na katika mechi za kirafiki amekosa mechi mbili za ligi kuu nchini humo ambayo imeanza hivi karibuni na majeraha haya yatamfanya akose mechi nyingi zaidi.

IBRAHIMOVIC ADAIWA KUMUWEKA ROHO JUU JOSE MOURINHO KUFUATIA KWA TAARIFA HII ALIYOITOA

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameendelea kumuweka roho juu meneja wake Jose Mourinho, kufuatia kuibua hoja ya kutaka kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu kwa mashar
Kwa muijibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Daily Mirror mapema hii leo zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo amegoma kusaini mkataba mpya hadi mwishoni mwa msimu huu, kwa lengo la kutaka kuona kama Man Utd itafanikiwa kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
Ibrahimovic ametangaza msimamo huo, kutokana na hitaji la kutaka kurejea kwenye michuano mikubwa barani ulaya ambayo hakuwahi kuikosa alipokua akizitumikia klabu za PSG, Inter Milan, AC Milan na FC Barcelona.
Hata hivyo, gazeti hilo halijaeleza ni wapi mshambuliaji huyo kutoka nchini Sweden atakapoelekea kama ataendelea na msimamo wake wa kutosaini mkataba mpya hadi mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wake wa sasa utakua unafikia kikomo.
Ibrahimovic alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Man Utd mwanzoni mwa msimu huu akiwa mchezaji huru, na mpaka sasa ameonyesha kusaidiana na wenzake ili kufikia lengo la kuipaisha Man Utd ili imalize katika nafasi nne za juu katika ligi ya England.
Majuma mawili yaliyopita Ibrahimovic alihusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuelekea nchini Marekani kujiunga na Los Angles Galaxy, lakini wakala wake alipoulizwa kuhusu uvumi huo hakuzungumza lolote zaidi ya kuwataka waandishi wa habari kusubiri hadi mwishoni mwa msimu huu.
Tayari mshambuliaji huyo ameshaifungia Man Utd mabao 17 katika michezo 27 aliyocheza tangu mwanzoni mwa msimu huu.

KLOPP AFUNGUKA JUU YA MADAI HAYA YAKUTAKA NAFASI ZA ULAYA

Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema hana budi kuelekeza nguvu zake katika nafasi nne za juu, baada ya kushindwa kufikia lengo la kuingia kwenye mbio za ubingwa kuelekea mwishoni mwa msimu huu.
Klopp amezungumza na vyombo vya habari na kukiri jambo hilo, ambapo amesema kuna haja ya kuanza kujielekea katika mfumo wa kusaka namna ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.
“Nitaridhika sana endapo nitaiwezesha Liverpool kumaliza nafasi nne za juu, lengo langu kubwa tangu mwanzoni mw amsimu huu lilikua hapa, japo tulionekana kuwa na nia ya kuufukuzia ubingwa wakati fulani, lakini kwa sasa mambo yamekwenda ndivyo sivyo.
“Inanilazimu kurudi katika lengo langu na nitahakikisha kila hatua tunayoipiga katika michezo iliyosalia tunafanikisha ushindi ili kusalia katika lengo letu. Najua lengo hili litakua ni furaha kwa kila mmoja wetu, kwa sababu tutakua tumeingia kwenye mpango mwingine wa kupambana barani Ulaya.”Amesema Klopp.

DYABALA AIANGAMIZA FC BARCELONA NCHINI ITALIA ,BAYERN MUNICH DHIDI YA REAL MADRID LEO PATAWAKA

USIKU wa ulaya,Uefa Champions League umeendelea kwa mchezo mmoja uliopigwa nchini katika ya wenyeji Juventus dhidi ya Fc Barcelona ya Hispania.
Mchezo uliotawaliwa na kasi kwa timu zote mbili lakini Barcelona walizidiwa baada ya mshambuliaji wao wa Juventus Paulo Dybala kuipatia timu yake magoli mawili ya mapema na kuwatoa mchezoni klabu ya Barcelona.

Kipindi cha kwanza kikamalizika kwa Juventus kwenda mapumziko na goli 2-0,lakini bado kipindi cha pili kuanza Juventus wakafanikiwa tena kupata goli la 3 kutoka kwa Chiellini.

Leo itapigwa michezo jumla mitatu na ule mmoja ambao ulihairishwa siku ya Jana Kati ya Borussia Dortmund dhidi ya As Monaco kutokana na sababu za kiusalama zaidi mara baada ya kutokea mlipuko karibu na basi me wachezaji wa Dortmund,hata hivyo katika mlipuko huo beki we wa Dortmund Bartra alikimbiwa hospitali baada ya tukio hilo.
Michezo mingine ni ule wa Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Atletico Madrid dhidi ya Leicester City.

RATIBA YA MECHI ZA LEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE

▪Champions League - Quarter-finals.

☆Borussia Dortmund Vs Monaco
Muda: 1:45 Usiku.

☆Atletico Madrid Vs Leicester City
Muda: 3:45 Usiku.

☆Bayern Munich Vs Real Madrid
Muda: 3:45 Usiku.


MATOKEO YA MECHI ZA JANA

☆Juventus 3-0 Fc Barcelona.

Yanga yawakalisha Waarabu wa Algeria.

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, Yanga SC wamepata ushindi w goli 1-0 dhidi ya MC Aalger mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.

Goli pekee la Yanga limefungwa na kiungo raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko dakika ya 61 kipindi cha pili baada ya kuwekewa pasi na Chirwa ndani ya eneo la 18 la MC Alger, Kamusoko hakuwa na papara na akaukwamisha mpira wavuni kwa kumuuza golikipa wa Alger.

Yanga ilistahili ushindi mkubwa kwenye mchezo wa leo lakini umakini wao mdogo ndio umewanyima ushindi mnono kwa sababu ya kushindwa kuzitumia nafasi nyingi ambazo zilitengenezwa kipindi cha kwanza.

Kuingia kwa mshambuliaji Donald Ngoma kuliimarisha zaidi safu ya ushambuliaji ya Yanga akisaidiana na Obrey Chirwa ambaye alikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mchezo wa leo licha ya kukosa nafasi kadhaa alipiga kichwa ambapo mpira uligonga mwamba.

Kama ilivyo kawaida wa timu za ukanda wa Kaskazini mwa Afrika, wachezaji wa MC Alger walikuwa wakijiangusha na kupoteza nafasi muda licha ya kuwa walikuwa nyuma kwa goli 1-0.

UKIACHANA NA SOKA, ZLATAN IBRAHIMOVIC ANATAMANI KUONEKANA KWENYE HIZI MOVIE

Kumbe Zlatan Ibrahimovic mbali na kuwa nyota wa Man united, anatamani pia kuwa muigizaji katika matoleo mapya ya movie James Bond na Jason Bourne.
Ndoto za Zlatan Ibrahimovic bado hazijafikia ukingoni kutokana na kwamba bado anaona anauwezo wa kuigiza kama James Bond au Jason Bourne  na sababu kubwa ikiwa ni kwamba mambo ya kuwa Secret Service anauweza vizuri.
Unahisi wapi Zlatan atatisha zaidi kati ya movie ya James Bond au Jason Bourne

Kuelekea mchezo kati ya Arsenal na Man City, tuyajue mambo haya 6.

  1.  Taarifa za timu, golikipa namba moja wa Arsenal Petr Cech anasumbuliwa na majeraha na mchezo wa mwisho zidi ya West Brom hakuwepo na uhakika wa kucheza dhidi ya City pia ni mdogo, Ozil pia ana majeraha huku kwa upande wa City “KDB” Kelvin De Bruyne hana uhakika wa kucheza kama ilivyo Sagna.
  1. Presha kwa pande zote mbili, sio Arsenal wala City wenye uhakika kubaki top four, Arsenal wanahitaji kumfunga City ili kujaribu kupanda juu huku City nao wanahitaji ushindi ili kutengeneza pengo la alama na wanaomfuatia.
  1. Wanaoweza kuanza. Arsenal Ospina,Monreal,Koscienly,Mustafi,Bellerin,Xhaka,Ramsey,Ozil,Walcott, Sanchez,Girod.
Man City Caballero,Clichy,Otamendi,Stones,Fernandinho,Toure,Sterling,De Bruyne,Silva,Sane,Aguero.
4.Mechi zilizopita.
Sep 2014, Manchester City 2 Arsenal 1.
Jan 2015, Manchester City 0 Arsenal 2.
Dec 2015, Arsenal 2 Manchester City 1.
May 2016, Manchester City 2 Arsenal 2.
Dec 2016, Manchester City 2 Arsenal 1.
  1. Mchezaji wa kuchungwa Arsenal, Alexis Sanchez amekuwa bora sana na tishio kwa wapinzani msimu huu, na ndiye mchezaji ambaye City watapaswa kumchunga sana, magoli 18 na asisst 9 msimu huu zinaonesha jinsi Mchile huyu alivyo wa kuchungwa.
  1. Mchezaji wa kuchungwa Man City, De Bruyne endapo akacheza mchezo huu anaweza kuwa tatizo kubwa kwa Arsenal, mara nyingi ana uono wa mchezo kwani anajua kufunga lakini pia anapiga pasi hatari sana na linaweza kuwa tatizo kwa Arsenal.

EMRE AANIKA NDOTO YAKE KWA REAL MADRID NA BARCELONA

Kinda Emre Mor wa Borussia Dortmund amesema ana ndoto za kuwa nyota mkubwa na kuweza kuichezea klabu ya Real Madrid.
Mchezaji huyo wa kimataiafa wa Uturuki alijiunga na klabu hiyo ya Bundesliga tangu mwezi Juni na ameishaitumikia Dortmund mara 15 katika mashindano ya msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 tu amekuwa na ndoto kubwa akiangalia matawi ya juu kuitumikia Real Madrid au mahasimu wao Barcelona.
“Dortmund ni moja ya timu kubwa duniani na ninajifunza mengi. Nataka kuichezea Real Madrid na kuwa nyota, ndoto yangu ni kuvalia jezi ya Real hata kama ni mapema sana,” alisema Emre.
Mor amekuwa akiipenda Madrid na kumuhusudu mshambuliaji Cristiano Ronaldo akionyesha hayo katika mchezo uliowakutanisha mwaka uliopita akiomba kubadirishana jezi na nyota wa miamba hiyo ya Hispania.

IBRAHIMOVIC AWASHUSHA PRESHA UNITED

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kuwa yupo katika mazungumzo na klabu yake ya Manchester United kuhusu kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kufuatia kiwango kizuri alichokionyesha.
Mshambuliaji huyo kutoka Sweden alisaini mkataba wa mwaka mmoja tu kuingia Man Utd akitokea Paris Saint – German katika msimu wa joto/kiangazi uliopita.
Amekuwa akihusishwa na habari za kutaka kutimkia Napoli au LA Galaxy lakini amethibitisha kufanya mazungumzo ya kutaka kuongeza mkataba mwingine.
“Ngoja tuone ila tunafanya mazungumzo, nina nafasi ya kuongeza mwaka mmoja, nataka kufanya vizuri kwa muda nitakao kuwepo hapa. Ngoja tuone itakavyokuwa” alisema Ibrahimovic.
Aliongeza kuwa anajivunia kuwa mchezaji wa Manchester United kwakuwa watu wengi wanatamani nafasi hiyo. Alisema watu wananihitaji awe katika klabu hiyo ambayo aliitaja kama klabu bora zaidi ya Uingereza.
Mkongwe huyo amefanya vizuri katika msimu wake wa kwanza akiwa na United akipachika mabao 26 kwenye mashindano yote huku mabao mengi akipachika katika ligi kuu nchini Uingereza.

AZAM FC KUMKOSA JOHN BOCCO

Klabu ya Azam itaendelea kumkosa nahodha na mshambuliaji wake tegemeo, John Bocco katika michezo minne mfululizo.
Daktari wa klabu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, alisema kuwa Bocco bado ni mgonjwa na atakuwa tayari kuanza mazoezi ifikapo Aprili 15 mwaka huu.
Mwankemwa alisema kutokana na hali yake kutoimarika, Bocco hataweza kuitumikia timu yake katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting.
“Pia Bocco hataweza kucheza katika mechi ya hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la FA dhidi ya Ndanda FC iliyopangwa kufanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wetu wa Azam Complex,”, alisema Mwankemwa.
Wakati huo huo, daktari huyo amependekeza mchezaji wa kimataifa wa timu hiyo Stephano Kingue, kupelekwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi.
Kikosi cha Azam ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame kinajiandaa kuwakabili Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa na matokeo yake yataonyesha mbio za ubingwa zinavyokwenda.
Simba ndiyo vinara katika msimamo wa ligi hiyo na endapo Yanga itafungwa au itatoka sare na wao kushinda Jumapili dhidi ya Kagera Sugar, watakuwa wamejiweka kwenye mazingira mazuri.

Majeruhi yaanza kuitesa Manchester United.

Hali sii hali ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na majeruhi yanayokiandama kikosi hicho, United wako katika mbio za kutafuta nafasi nne za juu katika ligi kuu ya Uingereza.
Mbio hizo zinaweza kuingia doa kwani hadi sasa wachezaji wa kikosi hicho 7 wanaweza kutokuwepo katika mchezo wao wa ligi mwishoni mwa wiki dhidi ya West Brom.
Hii inaweza kumpa mtihani kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ya juu ya nani aanze katika kikosi cha kwanza. Zlatan Ibrahimovich atakuwa anamaliza adhabu yake ya kadi nyekundu huku Ander Herrera naye akitumikia adhabu.
Phil Jones aliumizwa na Chris Smalling katika mazoezi ya timu ya taifa huku Smalling naye akiumia wakati akiwa na timu ya taifa. Kiungo wa timu hiyo Paul Pogba naye bado anauguza majeraha aliyoyapata kabla hata ya mechi za mataifa kuanza.
Marouane Fellaini naye bado ni majeruhi huku Wayne Rooney naye akiendelea kupona maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yalimfanya atoswe katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.
Matatizo ya kuumia kwa wachezaji muhimu yanaifanya United kuonekana kama wana kikosi finyu hali inayopelekea matajiri wa United kutaka kuongeza majina makubwa mwishoni mwa msimu.
Tayari United wanasemekana kumalizana mazungumzo ya awali na Antoine Griezman wa Atletico Madrid, lakini pia kukiibuka tetesi mpya kwamba United wanamtaka kwa nguvu zote nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar.

Luis Enrique: Barcelona always believed they could beat PSG

Luis Suarez and Neymar celebrate Sergi Roberto's dramatic goal against PSGLuis Suarez and Neymar celebrate Sergi Roberto's dramatic goal against PSG
Barcelona head coach Luis Enrique said he "never stopped believing" during a sensational Champions League win over Paris Saint-Germain on Wednesday night.
Having lost the first leg of the last-16 tie 4-0, Barca had given themselves hope when they pulled it back to 4-3 on aggregate at the Nou Camp, only for Edinson Cavani to score an away goal in the 62nd minute.
That looked as though it would send PSG through until a dramatic late comeback in the final minutes that saw Neymar score twice and then Sergi Roberto snatch victory with almost the last kick.
       

Luis Enrique celebrates Barcelona's victory over Paris St-Germain
Luis Enrique celebrates Barcelona's victory over Paris St-Germain
"I was brought to my knees," said Luis Enrique, who recently announced he is leaving at the end of the season,.
"I would like to thank everyone who kept their faith after we lost 4-0. This is dedicated to them because this isn't the Harlem Globetrotters, this is football.
 

Total Pageviews