Yanga yawakalisha Waarabu wa Algeria. | HABARI ZA TOWN

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...

Yanga yawakalisha Waarabu wa Algeria.

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, Yanga SC wamepata ushindi w goli 1-0 dhidi ya MC Aalger mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.

Goli pekee la Yanga limefungwa na kiungo raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko dakika ya 61 kipindi cha pili baada ya kuwekewa pasi na Chirwa ndani ya eneo la 18 la MC Alger, Kamusoko hakuwa na papara na akaukwamisha mpira wavuni kwa kumuuza golikipa wa Alger.

Yanga ilistahili ushindi mkubwa kwenye mchezo wa leo lakini umakini wao mdogo ndio umewanyima ushindi mnono kwa sababu ya kushindwa kuzitumia nafasi nyingi ambazo zilitengenezwa kipindi cha kwanza.

Kuingia kwa mshambuliaji Donald Ngoma kuliimarisha zaidi safu ya ushambuliaji ya Yanga akisaidiana na Obrey Chirwa ambaye alikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mchezo wa leo licha ya kukosa nafasi kadhaa alipiga kichwa ambapo mpira uligonga mwamba.

Kama ilivyo kawaida wa timu za ukanda wa Kaskazini mwa Afrika, wachezaji wa MC Alger walikuwa wakijiangusha na kupoteza nafasi muda licha ya kuwa walikuwa nyuma kwa goli 1-0.
About Author
  • mwana habari Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Total Pageviews