Kinda Emre Mor wa Borussia Dortmund amesema ana ndoto za kuwa nyota mkubwa na kuweza kuichezea klabu ya Real Madrid.
Mchezaji huyo wa kimataiafa wa Uturuki alijiunga na klabu hiyo ya Bundesliga tangu mwezi Juni na ameishaitumikia Dortmund mara 15 katika mashindano ya msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 tu amekuwa na ndoto kubwa akiangalia matawi ya juu kuitumikia Real Madrid au mahasimu wao Barcelona.
“Dortmund ni moja ya timu kubwa duniani na ninajifunza mengi. Nataka kuichezea Real Madrid na kuwa nyota, ndoto yangu ni kuvalia jezi ya Real hata kama ni mapema sana,” alisema Emre.
Mor amekuwa akiipenda Madrid na kumuhusudu mshambuliaji Cristiano Ronaldo akionyesha hayo katika mchezo uliowakutanisha mwaka uliopita akiomba kubadirishana jezi na nyota wa miamba hiyo ya Hispania.
0 comments:
POST A COMMENT