JOSE MOURINHO anashawishika sana kumtaka Romelu Lukaku na Antoine Griezmann ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na wachezaji hao kuungana Zlatan Ibrahimovic Manchester United.
The Old Trafford boss ametenga kiasi kikubwa cha pesa (Mtonyo) wa £160million kwaajili ya kuimarisha kikosi chake na pia kumuacha kipenzi cha Manchester united Wayne Rooney ambae anajiandaa kuondoka Klabuni hapo..
Mourinho pia anataka kumfanya Ibra kuwa godfather mpya wa Old Trafford kwa kumuongezea mkataba mpya wa kumfanya mswedeni huyo kubaki OT kwa mwaka mwingine tena wenye thamani ya £10m.
The Special One kesho anaingia kwenye mchezo mgumu na wa muhimu watakapokutana na Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani OT ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya timu yake kurudi kwenye Champions League..
Wachezaji ambao Mourinho anawafukuzia kwa muda mrefu bila kukata tama ni Antonie Griezmann wa Athletico Madrid, Dili la mchezaji huyo litafanikiwa zaidi kama Manchester united wakifanikiwa kumaliza Top 4 kwenye Epl na kwenda Champions League.
.
Pia mchezaji mwingine ambae Jose anamfukuzia ni Romelo lukaku ambae alimpeleka West Brom kwa mkopo na baadae kwenda Everton wakati anaifundisha Chelsea kabla ya kutua kwa mashetani wekundu..
Swali ni moja tu kwako mdau wa Perfect255 Je, Jose Mourinho atafanikiwa zaidi kwenye kikosi chake akishawaongeza hawa wachezaji anaowataka???
0 comments:
POST A COMMENT