Kuelekea mchezo kati ya Arsenal na Man City, tuyajue mambo haya 6. | HABARI ZA TOWN

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...

Kuelekea mchezo kati ya Arsenal na Man City, tuyajue mambo haya 6.

  1.  Taarifa za timu, golikipa namba moja wa Arsenal Petr Cech anasumbuliwa na majeraha na mchezo wa mwisho zidi ya West Brom hakuwepo na uhakika wa kucheza dhidi ya City pia ni mdogo, Ozil pia ana majeraha huku kwa upande wa City “KDB” Kelvin De Bruyne hana uhakika wa kucheza kama ilivyo Sagna.
  1. Presha kwa pande zote mbili, sio Arsenal wala City wenye uhakika kubaki top four, Arsenal wanahitaji kumfunga City ili kujaribu kupanda juu huku City nao wanahitaji ushindi ili kutengeneza pengo la alama na wanaomfuatia.
  1. Wanaoweza kuanza. Arsenal Ospina,Monreal,Koscienly,Mustafi,Bellerin,Xhaka,Ramsey,Ozil,Walcott, Sanchez,Girod.
Man City Caballero,Clichy,Otamendi,Stones,Fernandinho,Toure,Sterling,De Bruyne,Silva,Sane,Aguero.
4.Mechi zilizopita.
Sep 2014, Manchester City 2 Arsenal 1.
Jan 2015, Manchester City 0 Arsenal 2.
Dec 2015, Arsenal 2 Manchester City 1.
May 2016, Manchester City 2 Arsenal 2.
Dec 2016, Manchester City 2 Arsenal 1.
  1. Mchezaji wa kuchungwa Arsenal, Alexis Sanchez amekuwa bora sana na tishio kwa wapinzani msimu huu, na ndiye mchezaji ambaye City watapaswa kumchunga sana, magoli 18 na asisst 9 msimu huu zinaonesha jinsi Mchile huyu alivyo wa kuchungwa.
  1. Mchezaji wa kuchungwa Man City, De Bruyne endapo akacheza mchezo huu anaweza kuwa tatizo kubwa kwa Arsenal, mara nyingi ana uono wa mchezo kwani anajua kufunga lakini pia anapiga pasi hatari sana na linaweza kuwa tatizo kwa Arsenal.
About Author
  • mwana habari Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Total Pageviews