Klopp amezungumza na vyombo vya habari na kukiri jambo hilo, ambapo amesema kuna haja ya kuanza kujielekea katika mfumo wa kusaka namna ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.
“Nitaridhika sana endapo nitaiwezesha Liverpool kumaliza nafasi nne za juu, lengo langu kubwa tangu mwanzoni mw amsimu huu lilikua hapa, japo tulionekana kuwa na nia ya kuufukuzia ubingwa wakati fulani, lakini kwa sasa mambo yamekwenda ndivyo sivyo.
“Inanilazimu kurudi katika lengo langu na nitahakikisha kila hatua tunayoipiga katika michezo iliyosalia tunafanikisha ushindi ili kusalia katika lengo letu. Najua lengo hili litakua ni furaha kwa kila mmoja wetu, kwa sababu tutakua tumeingia kwenye mpango mwingine wa kupambana barani Ulaya.”Amesema Klopp.
0 comments:
POST A COMMENT