DYABALA AIANGAMIZA FC BARCELONA NCHINI ITALIA ,BAYERN MUNICH DHIDI YA REAL MADRID LEO PATAWAKA | HABARI ZA TOWN

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...

DYABALA AIANGAMIZA FC BARCELONA NCHINI ITALIA ,BAYERN MUNICH DHIDI YA REAL MADRID LEO PATAWAKA

USIKU wa ulaya,Uefa Champions League umeendelea kwa mchezo mmoja uliopigwa nchini katika ya wenyeji Juventus dhidi ya Fc Barcelona ya Hispania.
Mchezo uliotawaliwa na kasi kwa timu zote mbili lakini Barcelona walizidiwa baada ya mshambuliaji wao wa Juventus Paulo Dybala kuipatia timu yake magoli mawili ya mapema na kuwatoa mchezoni klabu ya Barcelona.

Kipindi cha kwanza kikamalizika kwa Juventus kwenda mapumziko na goli 2-0,lakini bado kipindi cha pili kuanza Juventus wakafanikiwa tena kupata goli la 3 kutoka kwa Chiellini.

Leo itapigwa michezo jumla mitatu na ule mmoja ambao ulihairishwa siku ya Jana Kati ya Borussia Dortmund dhidi ya As Monaco kutokana na sababu za kiusalama zaidi mara baada ya kutokea mlipuko karibu na basi me wachezaji wa Dortmund,hata hivyo katika mlipuko huo beki we wa Dortmund Bartra alikimbiwa hospitali baada ya tukio hilo.
Michezo mingine ni ule wa Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Atletico Madrid dhidi ya Leicester City.

RATIBA YA MECHI ZA LEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE

▪Champions League - Quarter-finals.

☆Borussia Dortmund Vs Monaco
Muda: 1:45 Usiku.

☆Atletico Madrid Vs Leicester City
Muda: 3:45 Usiku.

☆Bayern Munich Vs Real Madrid
Muda: 3:45 Usiku.


MATOKEO YA MECHI ZA JANA

☆Juventus 3-0 Fc Barcelona.

About Author
  • mwana habari Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Total Pageviews