HABARI ZA TOWN: habari

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...
Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

BUNGENI KIMENUKA NI SAKATA WA MCHANGA WA MADINI!!

BUNGE limeingia siku ya nne jana kujadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18, huku wabunge kadhaa wakiraruana kuhusu ripoti ya pili ya kamati iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli, kuhusu mchanga wa dhahabau (makinikia) pamoja na mikataba ya madini.

Ripoti ya kamati hiyo pamoja na watu wengine  iliwataja baadhi ya vigogo wa Serikali kuhusika moja kwa moja katika kusaini mikataba mbalimbali ya madini na kupendekeza vyombo vya dola viwachunguze.


Waliotajwa na ripoti hiyo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  katika Serikali ya awamu ya nne kuanzia 2008 hadi 2012.

Mwingine ni aliyewahi kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kuanzia mwaka 1993 hadi 2005 na Dk. Dalaly Kafumu aliyepata kuwa Kamishina wa Madini katika wizara ya Nishati na Madini kati ya mwaka 2006 na 2011.

Aliyekuwa wakwanza kuchafua hali ya hewa bungeni ni Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), aliyemkatisha Ngeleja wakati akichangia bajeti hiyo aliyewataka wabunge wanyanyuke kwenye viti vyao ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika kupambana na wizi wa rasilimali za taifa.

Wakati Ngeleja akichangia, Haonga alisimama na kuomba kumpa taarifa Ngeleja ambapo alisema. “Naomba kutoa taarifa, mheshimiwa Ngeleja yeye ni miongoni mwa wabunge waliotajwa katika kashfa hii ya makinikia, anapokuwa anachangia atuambie uhusika wake katika hili”.

Kabla Ngeleja hajasimama kujibu hilo, Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa akiongoza kikao hicho jana asubuhi, Mussa Zungu, alisema hiyo siyo taarifa na hivyo kumtaka Ngeleja kuendelea na mchango wake.

Hata hivyo Ngeleja kabla ya kuendelea alisema: “Haonga mdogo wangu anajua kutuhumiwa si kupatikana na hatia, maisha yanaendelea.

“Sisi Bunge tumetoa pongezi kwa rais kwa kazi kubwa aliyofanya, tumpongeze mheshimiwa rais, kwa hali tuliyofikia tunahitaji usimamizi wa sera, nimekuwa waziri kwa miaka mitano, tungeanza utaratibu wa kawaida kuboresha mikataba ya madini ingetuchukua miaka mingi kufikia hapa,” alisema.

Naye Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma (CCM), akichangia bajeti hiyo alipigilia msumari wa moto kwa kusema waliohusika wote wakamatwe kabla ya kuhojiwa.

“Nampongeza Rais na Profesa (Nehemiah Osoro- Mwenyekiti wa Kamati ya pili ya makinikia), aliwataja watu waliosababisha matatizo, wengine wako CCM, tusema ukweli tuache mzaha.

“Wengine wanaweka katika twitter eti sihojiwi mpaka mahakamani, wengine tunawaheshimu, mzee wetu humu ndani anatwitt eti hawezi kuhojiwa hadi mahakamani, kila mwaka, kila tuhuma anatajwa kwani yeye ni nani?

“Kama kuna uwezekano wakamatwe washtakiwe, wanaotusumbua humu ni hao hao waliotajwa….. katajwa Ngeleja, katajwa Chenge, katajwa Kafumu” alisema Msukuma na kuendelea:

“Nimefuatilia taarifa zote hata Rais Magufuli alipomtumbua aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,..sijui kama yumo humu….nina hamu naye.

“Rais Magufuli alisema aliyaamini ma – vyeti, tuangalie uwezo wa mtu ikiwezekana mawaziri wafanyiwe usaili kabla ya kupata nafasi.

“Tunaamini madigrii mwisho wa siku tunakuta wezi, tufanye kitu cha msingi, tusiamini haya madigrii, kuamini haya madigrii kunatuletea matatizo, zile Phd zimerudi kwetu,”alisema Musukuma.

Alisema watu wengi hawana vyeti, hawana elimu, Katiba inasema ukitaka cheo fulani inataka elimu kubwa sasa wamefoji hayo madigrii, uwezo ni mdogo makaratasi makubwa.

Kubenea

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), alisema wabunge wa CCM wamezungumza mengi kwamba wapinzani hawaungi mkono hoja ya kukomboa rasilimali.

Alisema wapinzani hawapaswi kuingia kwenye lawama hizo kwakuwa hawahusiki katika mikataba yote kwani hawajawahi kuingia katika Serikali na kwamba kazi hiyo ni ya CCM.

“Sisi hatuhusiki katika mikataba yote iliyofungwa, hatujawahi kuingia katika Serikali, hii ni kazi ya CCM…ni dudu lao wameliamsha wahangaike nalo.

“Imekuwepo hoja ya msingi kwamba eti tumeibiwa katika rasilimali zetu, tumeibiwa na watu waliokuja kuwekeza, mikataba ilifungwa kwa sheria zilizopo, walifunga mikataba… bahati mmoja wao kazungumza hakamatiki.

“Rais alikaa na aliyemwita mwizi jana, mlango wa Ikulu jana ulifunguliwa ukawa wazi mwizi akaingia Ikulu,” alisema.

Mange kimambi amtolea povu zito POLEPOLE!!!

Baada ya Pole pole kuandika hiyo post hapo juu ikiwa imemtaja Mange Kimambi, Mange akaamua kumtolea  uvivu kama ifuatavyo :
.
#Regrann from #mangekimambi_ - :

"PolePole Tokea uwe katibu uenezi wa CCM ile brain ya kuongea mapoint mazito mazito imetoweka kabisa Yani. Hivi PolePole unakumbuka ulivyokuwaga unawa-inspire watanzania kwa jinsi ulivyokuwaga unaongea mapoint mazitoooooo. Siku hizi unaongea kama Bashite. Huna point, unajibu vitu bila busara, unajibu mambo kiwepesi wepesi...
.
.
Hivi Kweli Polepole kweli kati ya yote niliyosema point kubwaaaaa uliyoiona wewe ni Mimi kusema Kinana ameacha kufanya kazi za Chama???? And it's 100% true kinana amegoma kufanya mambo ya chama mpaka Baba Bashite A.k.a mwenyekiti wa CCM akamueleze why alimuitia TISS. Kinana alishikiliwa Na TISS nyumbani kwake for over 2 weeks...
.
Kwa issue ya Kinana alivyokaaa vibaya kwa Sasa ilibidi nyinyi kama chama muwatoe hofu wana CCM Na watz kwa ujumla kwa kuweka wazi data kuwa siku ile Rais anasema kamtuma kinana india kwa matibabu Ni kweli alikuwa india mtaje na hospitali aliyokuwa amelazwa, aliondoka TZ tarehe ngapi kwa ndege gani Na alirudi lini after that itakuwa easy watu kuhakiki habari hizo..
.
.
Polepole naomba uongeeee hadharani kuwa Kinana hakuita mkutano na waandishi siku ile Na kwamba Hakuzuiliwa Na TISS nyumbani kwake na kwamba hakutolewa silaha na Tiss. Na kwamba hakuwahi kuwa under house arrest chini ya TISS.Hiyo ndo response Watanzania wanayoitaka Na sio unatoa Majibu mepesi mepesi yasiyo Na point like je nikokuonyesha picha za kinana akifabya kazi za chama utanipa nini? Yani umejibu ka mtoto wa miaka mitano. That's a shallow answer to such a deep issue? Tena kutoka kwa mtu uliekuwaga unachambua mambo kwa kina, ukituonyesha picha za zamani ukasema ni za recent tutajua vipi? Ndo maana nakwambia umetoa majibu shallow. Na kama alifanya lazma kulikuwa na media tuonyeshe link tukaangalie sio picha zako wewe za kuchomoa chini ya godoro, tunataka picha zilizokuwa released Na media. Ukinionyesha hizo ntakupa hii account iwe account ya CCM.
.
.
Kama wewe kweli unajiamini jibu mambo ya TISS. Najua you can't do that sababu ni ukweli Na unaogopa siku Kinana au Nape wakiamua kufunguka utaaibika so huwezi shubutu kusema Tiss hawajawahi kumzuia kinana..CCM jibuni issue ya TISS kumshikilia Kinana, sio mnakuja namajibu ya KiBashite." Mange Kimambi

MANGE AFUNGUKA HAYA KUHUSU INSTAGRAM YAKE!!!

Nimetumia a few days kufikiria ushauri mlionipa, jinsi gani naweza kuendelea kuspend all my time doing what I LOVE to do and at the same niweze kumsaidia Baba Kenzo kulea watoto.Sina choice anyways, mahakama ishatoa uamuzi kuwa kuanzia May 1st watanichukulia Kama mtu mwenye minimum wage job 😳 niwe nayo hiyo kazi nisiwe nayo ntajijua mwenyewe na balaa langu la Ufreedom fighter 🤣🤣. Kuanzia May 1st malipo niliyokuwa napokea kutoka kwa mzungu kila mwezi yanapunguzwa kwa 30%-40%.
.
.
I would do this for free forever if I could but circumstances just won't let me.Napenda nachokifanya sababu usiku nalala usingizi mzuri knowing I am making a difference in the world, hata kama nika difference kadunchu but its still something.
.
.
Nimeufikiria sana ushauri wenu wa kutengeneza App but kuhamia kwenye App ni kupunguza kasi za harakati.It means lazma mtu alipe ndo aweze kusoma nachoandika!Mpaka hapo ntapunguza wasomaji!na pia ntapunguza uzito wa vitu navyoandika, itakuwa niko kibiashara zaidi na sio kuelemisha watu.Information nazotoa lazma ziwe free kwa Watanzania wote.Tayari mtu analipia bundle alafu nimlipishe App kila mwezi, haitokuwa sawa. Pia kuhamisha harakati kutoka Instagram tayari napunguza ongezeko la wasomaji!Insta ndo watz wengi walipo na bado wako wengi hawaijui account yangu nikisema nihame na nyinyi tu alafu nianze kuposti habari nunu nusu insta alafu zingine niposti kwenye app sitopata wasomaji wapya!
.
.
So nimeona niachane na idea yoyote iliyokaa kibiashara au ambayo mtu atalazimika kulipa kwanza ndo anisome.Nimeona harakati zangu ziendelee based on donations na sio malipo.Yani kwamba atakaeona anaweza kuchangia chochote ili kunikeep online 15 hours of the day atafanya, ambae hana sio akose kunisoma sababu hana.So harakati zangu zitakuwa powered by the people. Mtu atakuwa anaweza ku-donate anytime akijisikia yeye kwa amount anayoweza yeye.
.
.
Nimeamua kufungua a GoFundMe page, Pia will provide other means of donating Kama bank account, western union, pay pal etc.Kwa walioko TZ nitaprovide namba ya mwanaharakati mmoja mwenye jina lake kuweza kutuma donation.Maana nikitumia namba yangu au ya kajamba nani kina Bashite hawachelewi kuifungia au kuiletea figisu.

KIGWANGALLA Amjibu Haya Mange Kimambi ..Baada ya Mange Kupost Hali Mbaya za Hospitali Nchini..!!!

Hamis kigwangalla leo ameamua kufunguka kwa mwanaharakati Mange Kimambi huko Instagram baada ya mwanadada huyo kupost picha na maombi kibao kutoka kwa wananchi wakimwomba awasaidie kufikisha vilio vyao serikalini.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya mwanadada Mange kufululiza kupost picha na post mbali mbali zikionyesha hali mbaya ya huduma za afya kwenye baadhi ya hospitali zetu.

Nyingi ya post zinaonyesha jinsi wanawake kwenye baadhi ya hospitali kubwa ( including MUHIMBILI ) wakiwa wamelala chini sakafuni na watoto wao baada ya kutoka kujifungua, na baadhi ya post nyingine ni message anazotumiwa na watu mbalimbali wakilalamika jinsi wanavyopata tabu kupata huduma za afya mahospitalini .

Watumishi 52,436 kuajiriwa


SERIKALI inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, watarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu.

Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).

“Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti.

“Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi ya watu 9,700 na tutaendelea kufanya hivyo, na hivi karibuni Rais amebariki kuajiriwa kwa madaktari wapya 258 na Jumatatu (keshokutwa) wanaripoti kazini.

Tutaendelea kuajiri na wataalamu wa kada nyingine, kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha mwezi Juni tutakuwa tumejiajiri kwa idadi tutakayoipanga kwa awamu, na katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuajiri watumishi wengine wa umma zaidi ya 52,436,” alisema.

Hata hivyo, alisisitiza Serikali itahakikisha hairudii makosa ya kuajiri watumishi hewa, wasio na sifa na weledi unaohitajika. Alisema kwa kiasi kikubwa uhakiki wa watumishi wa umma kwa ujumla umekwisha, lakini kazi hiyo ni endelevu, kwani serikali itaendelea kufanya hivyo mara kwa mara.

Alisema matunda ya uhakiki wa watumishi wa umma umebaini watumishi hewa 19,708 na ambao wameshaondolewa katika orodha ya mishahara ya watumishi wa umma. “Hawa wangeachwa, Serikali ingekuwa inapoteza kiasi cha Sh bilioni 19.8 kila mwezi, lakini fedha hizi zimeokolewa kupitia uhakiki wa watumishi wa umma.

Tunafanya haya kwa nia njema. Mathalani tusingewatoa hawa, si wangeziba nafasi za ajira za wengine na fedha ngapi zingepotea?” alihoji. Alisisitiza kuwa, wizara hiyo itaendelea kutimiza majukumu yake kwa vitendo ili kurejesha nidhamu ya serikali na utumishi wa umma kwa kuongeza uwazi na kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi wa watumishi wa umma ili wawajibike kwa wananchi ambao ndio wateja na waajiri wakuu wa watumishi wa umma.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa, alikemea tabia ya maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.

Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi. Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,” alisema Simbachawene

Waziri Majaliwa Kaagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya 4×4 Tanzania Limited Akamatwe

Waziri Majaliwa wa kwanza (kulia) akizungumza jambo.WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema timu aliyoiunda ichunguze tuhuma za ubadhirifu kwenye Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) imekamilisha kazi yake na imebaini madudu mengi zaidi.
Machi 16, 2017, Waziri Mkuu aliivunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora awakamate viongozi wanne wa pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa fedha za chama hicho utakapokamilika.
Waziri Mkuu ambaye amefanya ziara ya siku moja mkoani Tabora, ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 15, 2017) wakati akizungumza na wajumbe zaidi ya 300 wa mkutano wa wadau wa zao la tumbaku katika ukumbi wa Kiyungi mwana Isike, mjini Tabora.
“Nilikuja Tabora mara ya kwanza ili kuchukua hatua za dharura na leo nimekuja kuendelea na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuwezesha kilimo cha tumbaku kiwe na tija kwa wakulima na ndiyo maana niliomba wakulima, wanunuzi wa tumbaku, vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) na viongozi wa Serikali wawepo kwenye mkutano huu,” amesema.
Akitoa mrejesho juu ya uchunguzi uliofanywa na timu aliyoiunda, Waziri Mkuu amesema WETCU haikuwa na kitengo cha ununuzi kwa zabuni.
“Waliunda kampuni inayoitwa FDTU (Flu and Dark Tobacco Union) ambayo ni Umoja wa Wenyeviti wa Union zote za Tumbaku nchini ambayo ilipewa kazi zote za ununuzi wa pembejeo na hela walikuwa wanagawana,”amesema.
“Tumefanya ufuatiliaji hadi katika benki lakini kwenye akaunti hakuna hela mpaka sasa. Tumeangalia chanzo cha fedha za union zenu na kubaini hakuna fedha zinazotoka FDTU kwenda WETCU,” ameongeza.
Akifafanua kuhusu kashfa ya ununuzi wa gari aina ya shangingi lenye namba za usajili T181 DEN ambao ulifanywa kinyume na maazimio ya mkutano mkuu, Waziri Mkuu amesema viongozi wa WETCU walitumia zaidi ya sh. milioni 220 kuzidi kiwango kilichoidhinishwa na Mkutano Mkuu cha kununua gari lenye thamani ya sh. milioni 40.
“Gari walilolinunua ni la mwaka 2008 na siyo la mwaka 2015 kama taarifa zinavyoonesha. Lilikwishatumika kwa kilometa zaidi ya 95,000 lakini likarekebishwa hadi kubakiza kilometa 16,000 ili lionekane ni jipya,… maana yake wamekula fedha nyingi sana na ni lazima tuwachukulie hatua za kisheria kwa sababu wamekula fedha, wamenunua gari lililotumika na siyo maamuzi ya mkutano mkuu.”
Waziri Mkuu ameagiza Mkurugenzi wa kampuni ya 4×4 Tanzania Limited, Bw. Faraz Yaseen naye akamatwe na kuhojiwa ni kwa nini alihusika na kuuza gari la mwaka 2008 lakini akabadilisha nyaraka ili lionekane ni la mwaka 2015.
Akitoa ufafanuzi kuhusu uuzaji wa hisa za WETCU, Waziri Mkuu amesema chama hicho kilikuwa na hisa milioni 36 ambapo kilitoa milioni sita ili ziuzwe na zikapatikana sh. bilioni 2.520 na ndiko huko walitoa fedha za kununulia gari na vifaa vya ofisi kwa sh. milioni 49.
“Walichukua hisa 100,000 na kuziuza na wakapata sh. milioni 250 lakini fedha hizo hazikuwekwa kwenye akaunti ya chama. Hisa zilizobakia, ambazo ni milioni 30, walishaanza mchakato wa kuuza hisa milioni 28. Je mliahsatoa kibali Wamempatia cheti halisi cha hisa hizo wakala Zani Security ili auze hisa hizo bila kuomba kibali cha Mkutano Mkuu,” amesema.
“Kwa vile hawakupata idhini ya Mkutano Mkuu, na wala hawakufuata taratibu, kanuni na sheria, kuanzia leo nimesitisha mauzo ya hisa hizo na kirudishwe Tabora mapema iwezekanavyo. Mrajisi fuatilia Zani Securiy warudishe kile cheti kinachowapa dhamana ya kuuza hizo hisa.”
Waziri Mkuu amesema, kwa vile WETCU ina madeni mengi katika benko za CRDB na NMB, viongozi wa chama hicho waliamua kufungua akaunti mpya za fedha za kitanzania na dola za Marekani kwenye benki ya EXIM. Walifungua akaunti ya muda maalum na kuweka huko fedha ambazo zilishalisha faida ya zaidi ya sh. milioni 14 katika kipindi cha miezi mitatu.
“Ninamuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika kupitia COASCO (Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika) ya Tabora afuatilie benki ya EXIM hapa Tabora ili kubaini ni akina nani walikuwa wakifanya miamala hiyo,” amesema,
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama; Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba; Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa huo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA,
JUMAMOSI, APRILI 15, 2017

Maneno 20 ya Kusisimua Aliyoyasema Nape Nnauye Ijumaa Kuu..!!!


 Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye asubuhi ya jana ametuma ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter akisema Leo ni Ijumaa Kuu!Yesu Kristo alibeba machungu yote!Tusamehe wote waliosababisha machungu maishani mwetu! Tumshukuru Mungu kwa kila jambo!

CAG Afichua Ufisadi Mkubwa Serikalini..Aeleza Jinsi Misamaha ya Kodi Inavyoitafuna Nchi..!!!

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad, imebaini kuwapo kwa matumizi mabaya ya msamaha wa kodi wa shilingi bilioni 3.46, uliotolewa kwa walengwa wawili walioagiza jumla ya magari 238 mwaka wa fedha wa 2015/16.

Akiwasilisha ripoti ya matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 katika mkutano wa saba na kikao cha saba cha Bunge, Prof. Assad amesema, msamaha huo wa kodi ulitolewa, lakini magari hayo yalisajiliwa kwa majina ya watu tofauti na wale waliopewa msamaha.

Hata hivyo, amesema walengwa wote waliopewa msahaa huo walikana kuhusika na magari hayo, hali inayoonyesha bado kuna uhitaji wa kuboresha udhibiti na ufuatiliaji wa masuala ya misamaha ya kodi.

Katika udhibiti wa misahaha ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya migodi, Prof. Assad amesema katika ukaguzi walioufanya Mei 31, mwaka jana, wamebaini lita za mafuta 4,248,802 yaliyosafirishwa kutoka jijini Dar es salaam kati ya Oktoba 2014 na Disemba 2015 kwa ajili ya matumizi ya mgodi wa Buzwagi, Bulyankulu na Geita, nyaraka za uthibitisho hazikuweza kufika vituo husika na kuonesha mafuta hayo yaliyosamehewa kodi yalitumika tofauti na makusudi.

Pia hiyo imebaini lita 20,791,072 za mafuta yenye msamaha wa kodi wa shilingi bilioni 10.17 kwa ajili ya mgodi wa Buzwagi katika kipindi cha miezi 18 kuanzia Julai 2014 hadi Disemba 2015, yalisafirishwa kwenda kampuni ya M/S Agreeko mkandarasi msaidizi ambaye hakuwa mhusika wa msamaha huo.

Kutokana na matumizi hayo mabaya ya msamaha wa kodi, Prof. Assad ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa mafuta yote ambayo hayana ushahidi kama yamesafirishwa vituo vya uchimbaji madini na kukusanya kodi inayodaiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.599 na kodi ya shilingi bilioni 10.17 iliyosamehewa na kupelekwa kwa wakandarasi wasiohusika na msamaha huo.

Aidha, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha usimamizi unaimarishwa juu ya matumizi ya misamaha inayotolewa kwa mujibu wa sheria ili kuepuka hasara kwa serikali kutokana na matumizi mabaya ya misamaha ya kodi

KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE IMEMKUMBUSHA ALBERTO MSANDO JAMBO HILI

Baada ya Roma kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ishu ya mkasa walioupata wa kutekwa na watu wasiojulikana huku maelezo mengine yakiwa yanasubiriwa kufanyiwa upelelezi kwa ajili ya majibu zaid, mwanasheria Alberto Msando afunguka kuhusu kauli ya Waziri Mwakyembe.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari ambao ulihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa ajili ya kusikiliza situation nzima ilivyokuwa kuhusu Roma, wakati ilipofika nafasi ya Mh Dkt Harrison Mwakyembe kuzungumza, kuna moja ya kauli aliitoa akisema kwamba ‘Naomba wasanii, pale ambapo utakuta mtu wa ajabu anakuhoji, nipigie hata simu’ Sasa kauli hiyo ilimfanya mwanasheria Alberto Msando kutumia kurasa yake ya Instagram kuandika ujumbe.
Kupitia kurasa yake ya Instagram, Alberto Msando aliandika Hii kauli imenifanya nikumbuke tangazo kwenye swimming pool ‘ukizama piga namba hii 0712444555’. 😂😂😂😂. Sasa huyo mtu wa ajabu atakuwa fala akuache upige simu😂😂😂. Haki ya nani kuna vitu ukivifikiria unaweza ukajikuta kanisa la ufunuo na uzima unadeki!! Sasa hao walio ‘like’ wame ‘like’ nini? 😂😂😂. Mimi nimechoka. Na wewe @dogojanjatz umechekelea nimeona tweet yako, sasa unaetakiwa angalau umpigie simu ni Waziri wa Habari au Waziri wa Mambo ya Ndani? Kwa hiyo unachekelea kwamba Nesi akihojiwa na mtu wa ajabu ampigie Waziri wa Afya sio? Na Mwalimu akihojiwa na mtu wa ajabu ampigie Waziri wa Elimu? 😡😡. Dereva wa Bodaboda akihojiwa ampigie Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji?? #StressTu #TheDon

MBUNGE Halima Mdee Katika Kumi na Nane za Gwajima...Amtaka Akamuombe Msamaha

Leo Askofu Gwajima amemuongelea Halima Mdee katika Mahubiri yake na amemtaka Mbunge huyo kuacha mara moja kumtukana Spika akiwa Bungeni maana ni moja ya Mhimili wa Dola.

Amesema kuwa Halima Mdee asipoomba msamaha kwa tukio la kumuita fala Spika basi Jumapili ijayo atamchapa ipasavyo.

Inasikitisha..Roma Afunguka Haya kwa Uchungu Mara Baada ya Kupatikana Jana Usiku...!!!!

Hatimaye msanii Roma Mkatoliki akiwa na wenzake watatu amezungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza kufuatia tukio la kutekwa na watu wasiojulikana kwa takribani siku tatu.

Roma na wenzake wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari baada ya kutoka katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, walikoenda kupimwa afya zao baada ya kuhojiwa kwa takribani saa sita katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Msanii huyo amewashukuru watanzania kwa ushirikiano wao waliouonesha na kuwahakikishia kuwa wako salama kiafya. Alisema ingawa hajaingia kwenye mitandao lakini ameelezwa juhudi zilizofanywa na watanzania.

“Niwahakikishie mimi ni mzima kabisa mpaka sasa hivi, niko salama kiafya na hata kiakili. Na hata wenzangu watatu, Moni, Laden na Imma… niwahakikishie kabisa kuwa sisi wote ni wazima na tunaendelea vizuri,” alisema Roma na kuomba wapewe nafasi kwanza wakapumzike.

Aliongeza kuwa kwa sasa wako katika taratibu za kuelezea vyombo vya usalama kuhusu tukio zima la kutekwa kwao hivyo hawawezi kuweka wazi kwa umma kwa sasa.

Aidha, Roma ameahidi kuwa siku ya Jumatatu watazungumza na vyombo vya habari na kuueleza umma kuhusu undani wa kilichojili.

Roma na wenzake walitekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe Records ambapo watu hao walichukua pia vifaa vya studio hiyo ikiwa ni pamoja na ‘computer’ na runinga bapa, kwa mujibu wa mmiliki wa studio hizo.

Rasmi..Roma Mkatoliki Apatikana ..Kaka Yake Afunguka Alipokuwa..!!! kituo cha Polisi, Roma

Msanii Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki amepatikana na sasa yupo katika kituo cha Polisi cha Oyesterbay jijini hapa.

Kaka wa Roma,Omar Musa amesema Roma alirudishwa nyumbani saa tisa alfajiri leo, na kwa sasa yupo kituo cha Oyesterbay.

 Hata hivyo Omar hakutaka kueleza kwa kina kuhusu kurejea kwa Roma akisema kuwa hadi familia itakapotoa tamko.

Roma na wenzake wanne, walitekwa wakiwa katika studio za Tongwe, zilizopo Masaki, jijini hapa hivi karibuni.

Tesisi:Roma apatikana, yupo kituo cha Polisi Oysterbay


Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar.

Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.


Noma Sana..Husein Bashe Ashindwa Kuvuimilia..Afunguka Haya Mazito Kuhusu Sakata la Roma..!!!

Jana usiku taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.

Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma.

"Who is behind all this? Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu

“Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Taifa letu kama Mzee Karume na Mwl Nyerere, Tunawajibu wa kukataa ukandamizaji tukikaa kimya kwa kufikiri kuwa hayanihusu mimi yanamhusu yule yatakapokufika wewe hatakuepo mtu wa kukutetea na halitakuepo Taifa la Tanzania

“Sote tusimame tuseme hapana kwa mfumo huu unaoanza kuota mizizi kama mtu Ana makosa ufuatwe utaratibu wa kisheria kumkamata na sio utekaji tunakabiliwa na vita kubwa ya kupambana na Umasikini na kujenga Taifa huru la kiuchumi . 

"Umasikini ni hatari kwa usalama wa taifa sio nyimbo
#FreeRoma"

Kamanda Sirro Kukutana na Wasanii Jumamosi hii Kutoa Taarifa za Roma na Wenzie..!!!

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Jumamosi hii atakutana na wasanii kuwaeleza taarifa ya jeshi hilo kuhusiana na kupotea kwa rapper Roma Mkatoliki na wengine waliotekwa na watu wasiojulikana usiku wa Jumatano katika studio za Tongwe Records.

Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, Katibu Mkuu wa chama cha wasanii wa kizazi kipya, TUMA, Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Brighton amesema amefanikiwa kuongea na Kamanda Sirro Ijumaa hii.

“Yeye [Sirro] ametusisitiza kwamba tuendelee kuwa na uvumilivu hili suala wao wanalishughulikia, na bahati nzuri wao kama polisi wameshapata taarifa zetu, wameshafungua jalada,” amesema Brighton.

“Simon Sirro ametuhakikishia hilo, yuko na chombo, ameunda chombo maalum katika kuhakikisha kwamba hawa ndugu zetu wanapatikana salama. Na vile vile ametuahidi kesho saa tano na nusu wote kwa umoja wetu, wasanii pamoja na ndugu zetu waandishi wa habari tufike ofisini kwake pale ataweza kutupa taarifa ya hali inavyokwenda na wapi amefikia kama amewapata ama kuna taarifa yoyote kuhusu wao ambao wamepotea,” ameongeza.

Brighton ameiomba jamii kuwaunga mkono wasanii hao kuhakikisha Roma na wenzake wanapatikana wakiwa salama. Wengine waliopotea ni rapper Moni Centrozone, producer wa Tongwe Bin Laden wengine watatu.

Nape Nnauye Afunguka Haya Kwa Hisia Kali ..Sakata la Kutekwa kwa Roma..!!!

Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ilipotolewa taarifa kuwa msanii Roma Mkatoliki alitekwa na watu wasiojulikana akiwa pamoja na Moni Centrozone, mtayarishaji wa muziki wa Tongwe Records, Bin Laden katika studio za Tongwe Records, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemlilia msanii huyo.

Nape emetoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia mpendwa wake.

“Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.

 Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records, watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia muziki, kwenda kusikojulikana.

Mke wa Roma, Nancy ameeleza kuwa alifika katika vituo kadhaa vya polisi jijini Dar es Salaam kuulizia taarifa za mumewe, lakini alielezwa kuwa taarifa za Roma hazikuwepo.

Akizungumza kwa uchungu kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Nancy aliwaomba Watanzania kwa ujumla pamoja na vyombo vya usalama kusaidia kufahamu alipo mumewe.

Leo mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki, familia na ndugu wa Roma na wenzake

Kamanda Siiro Afunguka kuhusu kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki ..!!!

 
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa tayari wameshapata taarifa za kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, ‘Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki na kuongeza kuwa tayari timu yake ya upelelezi imeshaanza kazi.

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Katibu wa Chama cha Wanamziki wa Kizazi Kipya Tanzania, Samweli Mbwana alipotaka kujua kama Jeshi la Polisi lina taarifa ya kupotea kwa mwanamziki huyo.

Sirro amesema kuwa taarifa za kupotea kwa msanii huyo tayari wameshazipata na Jalada la upelelezi tayari limeshafunguliwa kwa ajili ya upelelezi.

Ameongeza kuwa timu yake ya upelelezi iko mtaani kwa ajili ya kujua kinachoendelea, na amewaomba wasanii na baadhi ya watu kutokuwa wepesi wa kusambaza uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake.

“Jamani mambo ya uvumi yaacheni, sio kitu kizuri unamvumishia mtu kitu ambacho hakijui na wengine wanasema kuwa Serikali inahusika kitu ambacho si cha kweli”,amesema Kamanda Sirro.

Aidha, Sirro amesema kuwa amepanga kukutana Waandishi wa Habari kesho saa tano Ofisini kwake ili kuweza kutoa ripoti kamili kuhusu kupotea kwa msanii huyo wa Bongo fleva kwani timu ya upelelezi tayari iko kazini.

Hata hivyo, amewatoa hofu wasanii na wananchi kwa ujumla kwamba suala hilo linafanyiwa kazi, hivyo hakuna haja ya kuogopa na kuendelea kuvumisha vitu visivyokuwa vya msingi.

WIZARA YA HABARI YATOA TAMKO KUHUSU KUPOTEA KWA MSANII ‘ROMA’

\
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa msanii aliyepotea, Ibrahim Mussa maarufu kwa jina la ‘Roma Mkatoliki’ kuwa anashikiliwa na Polisi.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zawadi Msalla imesema kuwa Wizara kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki huyo tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Katika taarifa hiyo, Msalla amesema kuwa Wizara imefuatilia kwa karibu suala hilo kwa kuwa lina mwelekeo wa kosa la jinai, hivyo amesema taarifa kutoka kwa vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.
Hata hivyo, Kutokana na uzito wa jambo hilo amesema kuwa, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuweza kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua mahali msanii huyo.

Ile Kesi ya Scorpion Mtoboa Macho Yafikia Hatua Hii..!!!

Mkazi wa Buguruni jijini hapa, Deus Johakim Magosa (45) ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi namba 303 ya mwaka 2016 ya kumjeruhi, kumtoboa macho na kumfanyia unyang’anyi wa kutumia silaha, Saidi Mrisho inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini, leo alinusurika kutupwa lupango baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga kumtuhumu kutoa ushahidi wa uongo.


Wakili Katuga alimtuhumu shahidi huyo  kutokana na kutoa majibu tofauti wakati akimuongoza kutoa ushahidi wake na maelezo aliyoyatoa awali Kituo cha Polisi cha Buguruni.

Awali shahidi huyo alisema mahakamani hapo kuwa hakuwahi kusikia popote kuwa Scorpion amehusishwa katika tukio la kumshambulia Said, lakini baadaye alipobanwa alisema ni kweli alisikia tetesi hizo kuwa mtuhumiwa huyo ndiye aliyefanya tukio hilo. Pamoja na mambo mengine aliyomhoji na kumbaini kuwa anatoa ushahidi wa uongo wakili Katuga

alipomgeukia hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Flora Haule  na kumwambia shahidi anazidi kuidanganya mahakama hiyo na kuitaka mahakama hiyo imchukulie hatua kwa mujibu wa kifungu cha 164 cha ushahidi hapa nchini (Tanzania Evidence Act).

Shahidi huyo alionekana kuwa katika wakati mgumu baada ya wakili huyo kuwaita askari polisi na kuwataka wakae tayari kumchukua shahidi huyo.

Hata hivyo kutokana na ufinyu wa muda hakimu Flora aliahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 18 mwaka huu na kumuacha shahidi huyo aondoke na kumtaka kufika tena mahakamani hapo tarehe iliyopangwa bila kukosa ambapo Scorpion naye alirudishwa mahabusu mpaka tarehe hiyo.

Mwandishi wetu alizungumza na mmoja wa wanasheria mahakamani hapo kuhusu ushahidi wa uongo ambapo, mwanasheria huyo alisema unapobainika kutoa ushahidi wa uongo ukiwa ndani ya kiapo unaweza kufungwa jela kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja.

Majaliwa: Hakuna aliye juu ya sheria.


SERIKALI imesema kuwa hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria na mamlaka ya kuwanyanyasa watu wasiokuwa na uwezo kwani Sheria haiangalii nafasi ya mtu.

Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliposimama kwenye Kijiji cha Miono wilayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya wananchi kudai kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakipendelewa mara wanapolisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Majaliwa alisema hakuna mtu aliyejuu ya sheria na kwamba watu wanapaswa kuzingatia sheria na wafugaji wanapaswa kufuga mifugo michache ambayo wataimudu na sio kufuga mifugo mingi huku eneo la malisho likiwa dogo.

Alisema kuwa watendaji wa serikali wanapaswa kutopendelea upande wowote ili haki iweze kutendeka na hakuna mtu atakayeonewa kisa uwezo wake ni mdogo.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Saadani kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na Hifadhi ya Saadani alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze na Mkuu wa wilaya na watu wa ardhi na kamati ya ardhi ya kijiji kwenda kwa ajili ya kuhakiki mipaka.

Majaliwa alisema kuwa ramani zipo hivyo hakuna sababu ya kugombana kwani kila kitu kinajulikana na haki itatendeka na wananchi hawataweza kuonewa.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema kuwa kumekuwa na migogoro mingi ya mipaka katika vijiji ambavyo vinapakana na Hifadhi hiyo hali ambayo imeleta uhasama mkubwa.

Ridhiwani alisema kuwa kamati mbalimbali za kusuluhisha migogoro hiyo zimeundwa na bado zinaendelea kufuatilia changamoto hizo hivyo anaamini kwenda kwake kutasaidia kuharakisha kufikia mwisho kwa migogoro hiyo.
 

Total Pageviews