Katika mkutano huo na waandishi wa habari ambao ulihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa ajili ya kusikiliza situation nzima ilivyokuwa kuhusu Roma, wakati ilipofika nafasi ya Mh Dkt Harrison Mwakyembe kuzungumza, kuna moja ya kauli aliitoa akisema kwamba ‘Naomba wasanii, pale ambapo utakuta mtu wa ajabu anakuhoji, nipigie hata simu’ Sasa kauli hiyo ilimfanya mwanasheria Alberto Msando kutumia kurasa yake ya Instagram kuandika ujumbe.
Kupitia kurasa yake ya Instagram, Alberto Msando aliandika Hii kauli imenifanya nikumbuke tangazo kwenye swimming pool ‘ukizama piga namba hii 0712444555’. 


. Sasa huyo mtu wa ajabu atakuwa fala akuache upige simu

. Haki ya nani kuna vitu ukivifikiria unaweza ukajikuta kanisa la ufunuo na uzima unadeki!! Sasa hao walio ‘like’ wame ‘like’ nini? 

. Mimi nimechoka. Na wewe @dogojanjatz umechekelea nimeona tweet yako, sasa unaetakiwa angalau umpigie simu ni Waziri wa Habari au Waziri wa Mambo ya Ndani? Kwa hiyo unachekelea kwamba Nesi akihojiwa na mtu wa ajabu ampigie Waziri wa Afya sio? Na Mwalimu akihojiwa na mtu wa ajabu ampigie Waziri wa Elimu? 
. Dereva wa Bodaboda akihojiwa ampigie Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji?? #StressTu #TheDon
0 comments:
POST A COMMENT