HABARI ZA TOWN: burudani

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...
Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

Msanii Linah Sanga afunguka haya kuhusu ujauzito wake!!!

Image result for linah sanga
Linah Sanga 'Ndege Mnana' amefunguka na kuweka wazi kwamba haoni tatizo yeye kupiga picha za kuachia tumbo lake lenye ujauzito wazi kwani picha ni za kawaida sana wala hazina matatizo yoyote. Linah amefunguka hayo kwenye kamera za eNewz na kudai kwamba hawezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wake huku akidai wakosoaji wapo wengi.

HARMORAPA Ajiita Strong Woman ...!!!

Rapa Harmorapa jana aliwaacha mdomo wazi baadhi ya mashabiki wake baada ya kutoa jibu tofauti kuhusu jinsia yake.

Akichat na mashabiki katika mtandao wa facebook wa EATV ndani ya kipindi cha  Kikaangoni, rapa huyo aliulizwa swali kuhusu jinsi yake "Wewe ni mwanaume wa aina gani?' na rapa huyo kujibu "Mimi ni strong woman".

Jibu hilo limewashangaza mashabiki wengi wa rapa huyo kwa kuwa wanajua yeye ni mwanaume huku wengine wakidhani huenda hakuelewa swali kutokana na lugha ya kingereza iliyotumiwa.

Akiongea kuhusu uwezo wake wa kuongea na kuandika lugha ya kingereza alisema: “Lugha ya Kiingereza naifahamu vizuri lakini ile kuongea ongea ndiyo siwezi”

Rapa huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Kiboko ya Mabishoo’.

Huu ndio ujumbe Rich Mavoko alioutoa kwa wasanii wote wa Tanzania…mpaka bosi wake Diamond

Rich MavokoRich Mavoko ana ujumbe na ni ujumbe ambao anaelekeza kwa wasanii wote Tanzania na pia mashabiki wake.
Na ni ujumbe ya kwamba anawachilia wimbo wake mpya na ina maana watu waache siasa na washughulike na kueneza wimbo huo.
Tunafikiri alikuwa akimweleza bosi wake Diamond ambaye amekuwa akihusika na mambo ya siasa sana Tanzania.
Huu ujumbe ulikuja pia na picha tunayo tumaini ni wimbo mpya aliotoa. Itakuwa wimbo wake mwingine baada ya Kokoro.
Hivi ndivo alivyoandika mitandaoni:
“Hapana, siasa ipo kila siku ila now naona wasanii wengi wanaliongelea hilo, ila mie sidhani kama ngoma nzuri inashindwa kwenda kwaajili ya siasa,” amesema.
Kuhusu muda wa kuachia wimbo wake Mavoko amesema, “Wiki hii naweza kufanya hivyo, au wiki ijayo mwanzoni.”
Na pia kutupa picha hii:Rich Mavoko

Hii ndio picha ya Zari akiwa bado fukara ambayo imezubaisha wengi…hata Diamond Mwenyewe

zariSaa hii Zari ako kwenye mitandaoni akionnyesha manguo, magari na maisha kiistaarabu lakini hakuanzia hapo.
Kuna wakati alikuwa msichana wa kawaida tu..mweusi na mwenye mavazi na nywele za kawaida tu and watu wachache sana wangetmani wakati huo.
Ameabadilika sana na kwa kweli alibleach uso wake ili kufanana na ma star wengine mpaka na wale wa marekani.
Ebu tazama hii picha:Zari

CHEKI 50 CENT ALIVYOSHUSHA NGUMI KWA SHABIKI WA KIKE

50 Cent aamua kuimalizia Gym kwa shabiki wa kike stejini.
Huwa anafahamika sana kwa mabeef na wasanii wenzake pale wanapokuwa wamevurugana, ila kwa hili,50 cent hakuwa na beef na rapper yeyote yule ila ni shabiki wake wa kike ambae alichezea ngumi ya maana.
Shabiki huyo wa kike alipewa ngumi ya kifua baada ya kumvuta 50 kutoka stejin wakati akiwa anaperforme, ila baada ya tukio hilo 50 cent akaona sio kesi akimpandisha huyo dada kwenye steji kujumuika nae.
50 sio msanii wa kwanza kumpiga mwanamke, Kevin Gates ni mojawapo na alihukumiwa kwenda jela kwa miezi 6 kwa kosa hilo.

Kimenukaa..Mange Afunguka Mazito..Adai Wakenya Wametumwa Kwenda Kumuua..Amtahadharisha Wema Sepetu..!!!

Wema tafadhali be very careful.,,,,, Hali ni mbaya! Bashite ana hasira na wewe na Bashite akikuchukia ujue na Mkulu automatically ameshakuchukia. So please Wema jiangalie sana!! Acha kualika watu nyumbani! Acha kutoka peke yako, Weka ulinzi mzuri nyumbani ikibidi weka CCTV cameras ambazo zina remote access.... Magufool na Bashite hawatopenda ufike kampeni za 2020 sababu wanaijua kazi yako ya kuhamasisha vijana!!! Jiangalie sanaaaaa mdogo wangu!!!
.
.
.
Hawa watu wana play by the Kagame playbook! Hakuna mtu anaemsema vibaya Kagame anaendelea kupumua! Sio alieyopo Rwanda au nje ya Rwanda! Ukifungua mdomo juu ya Kagame you are a dead man walking na hii ndo kitu Magufool na Bashite wanaileta Tanzania........
.
.
.
.
Mimi mwenyewe hapa Sasa hivi naishi roho mkononi najua anytime watanitungua Ila nifanyeje sasa? Hatutakiwi kuwaogopa... Cha maana nilichofanya niku- involve polisi kuwa my government wants to harm me so nachofanya nikucheck-in kila baada ya muda flani( siwezi kuutaja) na nisipocheck in tu wanajua nimepatwa na kitu......na nimeinstall cameras mbele na nyuma ya gari yangu Camera ambazo zinakuwa accesed remotely pamoja na mlangoni kwangu. Nachotaka angalau atakaeniua apatikane... Na nimeambiwa na watu wengi mnoooo kuwa watakaotumwa kuja kuniumiza wala sio Watanzania, ni Wakenya!! Hata Ulimboka ile issue ilifanywa na Wakenya.....Napia najua nikifa Mimi ataibuka mwingine kama Mimi au zaidi yangu Mimi..... Mbona Ben Saanane wamemuua na watu ndo kwanza tunapanga kulitifua upyaaaa timbwili la PhD ya mkulu na hatuogopiiiii?? . Kama wanataka watu wanyamaze basi wabadilike..... Ila sio kutuletea mambo ya Kagame....

Chanzo -  Mange kimambi Instagram Page

Erick Shigongo Aendelea Kuwapa Makavu Live Diamond na Uongozi Wake...Adai Wanajichimbia Shimo

Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma, aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo.
Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya.
Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno.
Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo katika ardhi yake ya nyumbani, lakini badala yake wamekuwa wakimuona mara nyingi akifanya shoo Marekani, Ulaya, Nigeria, Afrika Kusini, kwenye Mashindano ya Afcon na sehemu nyingine nyingi ambazo ni nje ya Tanzania, mahali alipozaliwa na kuthaminiwa, mahali ambapo aliweza kujijazia mashabiki wengi.
Mashabiki zake wanahitaji shoo, kumsoma kwamba amejenga nyumba, amenunua au amepata watoto na Zari si kitu ambacho mashabiki wanakihitaji zaidi kutoka kwake, wanachohitaji ni kuona shoo zake kwa wingi kama kilivyokuwa kipindi cha Moyo Wangu, Kamwambie na nyimbo nyingine.
Ni kweli ana jina kubwa, ana mashabiki wengi, amepambana sana kufika alipokuwa lakini kwa upande mwingine anatakiwa kuangalia gharama za shoo zake hasa anapofanya nchini Tanzania, kwa watu ambao walimfanya leo kujulikana zaidi kama Diamond na si Naseeb Abdul.
Leo, Diamond anafanya shoo kwa dola 55,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100. Hii inamaanisha kwamba kwa mtu kama mimi, nikimchukua Diamond kwa gharama hiyo inamaana kwamba nitataka niingize kiasi kikubwa kama faida, kwa hiyo badala ya kufanya shoo Dar Live, Diamond Jubilee au sehemu nyingine, nitaihamishia shoo yangu Mlimani City na kufanya kiingilio cha shilingi elfu hamsini.
Swali la kujiuliza, je, yule bodaboda anayepiga sana nyimbo za Diamond ataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini? Yule kijana anayatafuta riziki kwa kuingiza nyimbo za Diamond kwenye simu za wateja ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? 


Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza.
Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi. 
Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona?
Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza.
Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa.
Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo. Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU”
Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki.
TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!! MWISHO.

Pacha wa Wema: Mimi Kauzu, Simshobokei Wema!

Lisa Deedee `Tuerny’.
DAR ES SALAAM: Kuna imani kuwa duniani wawiliwawili! Hii inajidhihirisha kwa mwanadada Lisa Deedee `Tuerny’ ambaye amejipatia umaarufu mitandaoni kutokana na kufananishwa na staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu.
Kupitia gazeti hili, mrembo huyo anafunguka mambo mbalimbali usiyoyajua kuhusu yeye; Ijumaa: Hivi Tuerny ulijuaje kuwa unafanana na Wema?
Tuerny: Nakumbuka mwaka 2012 niliweka picha mtandaoni, mama akanitumia sms kwamba ninafanana na Wema, nilishtuka lakini tangu hapo akawa kama amebariki hicho kitu. Nilishangaa kila sehemu niliyokwenda watu wananiambia nafanana na Wema.
Tuerny.
Ijumaa: Ulijisikiaje kufananishwa naye na ni changamoto zipi unazokutana nazo?
Tuerny: Sikuona kama ni kero, nilichukulia kawaida tu, haikuwa chanzo cha mimi kufanya vitu vya kufanana naye, mimi siyo mtu wa shobo kama hao wengine na sijawahi kuwa shabiki wake, changamoto ni kwamba wengi wanajua Wema ni ndugu yangu wakati si kweli.
Wema.
Ijumaa: Je, umeshawahi kuwa na ukaribu na Wema?
Tuerny: Sijawahi na sifikirii, ila kipindi watu wanaanza kunifananisha naye alifurahi akawa ana-comment kwenye picha zangu Instagram, akawa ananisifia na mimi ninamjibu, lakini kutokana na maneno ya watu akachukia na kunipotezea.
Ijumaa: Kwa nini hupendi awe rafiki yako?
Tuerny.
Tuerny: Yeye ana marafiki wengi na kwenye maisha yangu sipendi kuwa na mtu mwenye marafiki wengi, kwani majungu yatakuwa mengi.
Ijumaa: Nilisikia kuna kipindi uliwahi kukutana na Wema lakini ukampotezea hata salamu hukumpa, kwa nini?
Tuerny: Ni kweli, mwaka 2015 nikiwa kwenye mishe zangu nilimuona pale Klabu Cafee, akatabasamu na mimi pia, tatizo mimi sijui kujipendekeza ndiyo maana sikumfuata.
Wema.
Ijumaa: Vigogo wangapi ambao wamewahi kukuomba penzi, kwa kutaka kuonja ladha ya copy ya Wema?
Tuerny: Inawezekana watu wanaumiza kichwa kwa sababu hiyo, lakini wanashindwa kunifuata kutokana muonekano wangu, mimi ni kauzu zaidi ya dagaa.
Ijumaa: Uliwahi kukumbwa na kashfa ya kutoka kimapenzi na Romy Jones, ilikuwaje?
Tuerny: Sijawahi kuwa naye, watu walizusha kwa sababu zao binafsi.
Ijumaa: Mfano Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ sukari ya warembo, akikutokea utakubali?
Tuerny: Hahaa siwezi, kuwa na mwanaume mpaka nimpende siyo tu kwa sababu yeye ni f’lani.
Ijumaa: Ni mwanaume wa aina gani anakidhi vigezo kuingia naye kwenye uhusiano?
Tuerny.
Tuerny: (anacheka) awe mrefu, mwenye bodi na anajielewa, yaani asiwe mtu wa kuongea sana, maana sipendi mtu muongo.
Ijumaa: Kuna mastaa ambao wameshawahi kukuomba penzi na ulishawahi kutoka na wangapi?
Tuerny: Wapo wengi wanaoshoboka, huwa nawapotezea na siwezi kuwataja kwa sababu sipendi kujikweza.
Ijumaa: Je, una ndoto ya kuwa msanii wa filamu au muziki au video queen?
Wema.
Tuerny: Mmh, kuwa video queen hapana labda mtu anilipe si chini ya milioni saba, kuhusu filamu labda niwe dairekta, ila ndoto yangu kubwa ni kuwa mwanamuziki, naamini itatimia ‘soon’.
Ijumaa: Unajishughulisha na nini, kinachoweza kukukwamua kimaisha?
Tuerny: Nina saluni yangu inaitwa T flawless ipo Magomeni-Mikumi ninapoishi, yaani make up studio, napamba maharusi na watu wa kawaida

Huyu Ndiye Mwakyembe Bwana..Soma Hapa Maneno Aliyompokea Nayo Nay a Mitego Baada ya Kufika Dodoma...Lazima Ucheke Aisee..!!!

Rapper Nay wa Mitego, Alhamis hii aliitikia wito wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kukutana naye mjini Dodoma kwaajili ya kuzungumza namna ya kuuboresha wimbo wake Wapo ambao licha ya kuikosoa vikali serikali pamoja na Rais Dkt John Magufuli umepokelewa kwa mikono miwili.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais Magufuli kuamuru kuachiwa huru kwa Nay ambaye alikuwa amekamatwa na polisi na wimbo wake kufungiwa na BASATA. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Dkt Mwakyembe alisema wasanii wana nafasi kubwa katika kuisaidia serikali kukemea mambo maovu.

Amewataka vijana kutambua kuwa Tanzania ni nchi inayozingatia utawala wa sheria na kwamba wana uhuru wa kukosoa bila kutukana au kwenda nje ya maadili. “Na ndio maana tukasema kwa wimbo wa Nay hapana, hebu ngoja tuusikie, mbona ni wimbo mzuri tu,” alisema Mwakyembe.

Baada ya Kuwa Kimya na Ubize wa Kunyonyesha Zari Aibuka Kivingine kwa Staili Hii Mpya..!!!

Changamoto kubwa aliyonayo mwanamke baada ya kujifungua mtoto ni kulirudisha umbo lake katika ubora wake
Na kwa wanawake ambao uzuri na muonekano wao ni kipaumbele cha kwanza, hali huwa tete zaidi. Lakini si kwa Mrs Chibu Dangote, Zari the Bosslady ambaye ameonesha kufurahia jinsi alivyorudi kwenye reli fasta.
Amepost picha za muonekano wake wa miezi mitatu na nusu tangu apate mtoto wa pili na Diamond na so far yeye mwenyewe anaridhika na maendeleo ya umbo lake huku pia akitoa tips kwa wanawake wengine.
“You can achieve it if you put your mind onto it then implement it. #HerbalLife #Snapback 3months and a half… yes you can do it,” ameandika kwenye selfie aliyoiweka Instagram.
Kwenye picha nyingine ameandika, “diets needed, am a typical African woman who loves her food, just learn how to eat right, exercise and drink lots of water for your skin.”
Hakuacha kuwapa ‘haters’ vidonge vyao pia, “They will need respirators trying to keep up with me. I have no brakes so I ain’t stopping soon @GrindMode.”
 

Total Pageviews