Changamoto kubwa aliyonayo mwanamke baada ya kujifungua mtoto ni kulirudisha umbo lake katika ubora wake
Na kwa wanawake ambao uzuri na muonekano wao ni kipaumbele cha kwanza,
hali huwa tete zaidi. Lakini si kwa Mrs Chibu Dangote, Zari the Bosslady
ambaye ameonesha kufurahia jinsi alivyorudi kwenye reli fasta.
Amepost picha za muonekano wake wa miezi mitatu na nusu tangu apate
mtoto wa pili na Diamond na so far yeye mwenyewe anaridhika na maendeleo
ya umbo lake huku pia akitoa tips kwa wanawake wengine.
“You can achieve it if you put your mind onto it then implement it.
#HerbalLife #Snapback 3months and a half… yes you can do it,” ameandika
kwenye selfie aliyoiweka Instagram.
Kwenye picha nyingine ameandika, “diets needed, am a typical African
woman who loves her food, just learn how to eat right, exercise and
drink lots of water for your skin.”
Hakuacha kuwapa ‘haters’ vidonge vyao pia, “They will need respirators
trying to keep up with me. I have no brakes so I ain’t stopping soon
@GrindMode.”
0 comments:
POST A COMMENT