HABARI ZA TOWN

HABARI ZA TOWN

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...

Latest Post

BUNGENI KIMENUKA NI SAKATA WA MCHANGA WA MADINI!!

BUNGE limeingia siku ya nne jana kujadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18, huku wabunge kadhaa wakiraruana kuhusu ripoti ya pili ya kamati iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli, kuhusu mchanga wa dhahabau (makinikia) pamoja na mikataba ya madini.

Ripoti ya kamati hiyo pamoja na watu wengine  iliwataja baadhi ya vigogo wa Serikali kuhusika moja kwa moja katika kusaini mikataba mbalimbali ya madini na kupendekeza vyombo vya dola viwachunguze.


Waliotajwa na ripoti hiyo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  katika Serikali ya awamu ya nne kuanzia 2008 hadi 2012.

Mwingine ni aliyewahi kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kuanzia mwaka 1993 hadi 2005 na Dk. Dalaly Kafumu aliyepata kuwa Kamishina wa Madini katika wizara ya Nishati na Madini kati ya mwaka 2006 na 2011.

Aliyekuwa wakwanza kuchafua hali ya hewa bungeni ni Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), aliyemkatisha Ngeleja wakati akichangia bajeti hiyo aliyewataka wabunge wanyanyuke kwenye viti vyao ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika kupambana na wizi wa rasilimali za taifa.

Wakati Ngeleja akichangia, Haonga alisimama na kuomba kumpa taarifa Ngeleja ambapo alisema. “Naomba kutoa taarifa, mheshimiwa Ngeleja yeye ni miongoni mwa wabunge waliotajwa katika kashfa hii ya makinikia, anapokuwa anachangia atuambie uhusika wake katika hili”.

Kabla Ngeleja hajasimama kujibu hilo, Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa akiongoza kikao hicho jana asubuhi, Mussa Zungu, alisema hiyo siyo taarifa na hivyo kumtaka Ngeleja kuendelea na mchango wake.

Hata hivyo Ngeleja kabla ya kuendelea alisema: “Haonga mdogo wangu anajua kutuhumiwa si kupatikana na hatia, maisha yanaendelea.

“Sisi Bunge tumetoa pongezi kwa rais kwa kazi kubwa aliyofanya, tumpongeze mheshimiwa rais, kwa hali tuliyofikia tunahitaji usimamizi wa sera, nimekuwa waziri kwa miaka mitano, tungeanza utaratibu wa kawaida kuboresha mikataba ya madini ingetuchukua miaka mingi kufikia hapa,” alisema.

Naye Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma (CCM), akichangia bajeti hiyo alipigilia msumari wa moto kwa kusema waliohusika wote wakamatwe kabla ya kuhojiwa.

“Nampongeza Rais na Profesa (Nehemiah Osoro- Mwenyekiti wa Kamati ya pili ya makinikia), aliwataja watu waliosababisha matatizo, wengine wako CCM, tusema ukweli tuache mzaha.

“Wengine wanaweka katika twitter eti sihojiwi mpaka mahakamani, wengine tunawaheshimu, mzee wetu humu ndani anatwitt eti hawezi kuhojiwa hadi mahakamani, kila mwaka, kila tuhuma anatajwa kwani yeye ni nani?

“Kama kuna uwezekano wakamatwe washtakiwe, wanaotusumbua humu ni hao hao waliotajwa….. katajwa Ngeleja, katajwa Chenge, katajwa Kafumu” alisema Msukuma na kuendelea:

“Nimefuatilia taarifa zote hata Rais Magufuli alipomtumbua aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,..sijui kama yumo humu….nina hamu naye.

“Rais Magufuli alisema aliyaamini ma – vyeti, tuangalie uwezo wa mtu ikiwezekana mawaziri wafanyiwe usaili kabla ya kupata nafasi.

“Tunaamini madigrii mwisho wa siku tunakuta wezi, tufanye kitu cha msingi, tusiamini haya madigrii, kuamini haya madigrii kunatuletea matatizo, zile Phd zimerudi kwetu,”alisema Musukuma.

Alisema watu wengi hawana vyeti, hawana elimu, Katiba inasema ukitaka cheo fulani inataka elimu kubwa sasa wamefoji hayo madigrii, uwezo ni mdogo makaratasi makubwa.

Kubenea

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), alisema wabunge wa CCM wamezungumza mengi kwamba wapinzani hawaungi mkono hoja ya kukomboa rasilimali.

Alisema wapinzani hawapaswi kuingia kwenye lawama hizo kwakuwa hawahusiki katika mikataba yote kwani hawajawahi kuingia katika Serikali na kwamba kazi hiyo ni ya CCM.

“Sisi hatuhusiki katika mikataba yote iliyofungwa, hatujawahi kuingia katika Serikali, hii ni kazi ya CCM…ni dudu lao wameliamsha wahangaike nalo.

“Imekuwepo hoja ya msingi kwamba eti tumeibiwa katika rasilimali zetu, tumeibiwa na watu waliokuja kuwekeza, mikataba ilifungwa kwa sheria zilizopo, walifunga mikataba… bahati mmoja wao kazungumza hakamatiki.

“Rais alikaa na aliyemwita mwizi jana, mlango wa Ikulu jana ulifunguliwa ukawa wazi mwizi akaingia Ikulu,” alisema.

Zitto Kabwe asema haya kuhusu serikali ya JPM kuhusu sekta ya viwanda

Image result for zitto kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameitaka serikali kusimamia ipasavyo sekta ya viwanda ili kuhakikisha kinachozalishwa nchini kinakuwa na maana kwa faida ya Watanzania,


Amehimiza serikali kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya kuvurugwa na bidhaa za nje ambazo zinaingizwa kinyemela, vinginevyo ikubali kuwa inaviua makusudi.

Zitto ambaye ni kiongozi mkuu wa Chama cha ACT –Wazalendo, alisema serikali imekuwa ikishindwa kusimamia ushauri inaopewa na wabunge, akitolea mfano wa alichokieleza bungeni wakati wa mkutano wa bajeti mwaka jana kuhusu umuhimu wa kulindwa viwanda vya ndani.

Alikuwa akichangia hoja ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri Charles Mwijage.

“Wito wangu kwenye hili bado ni uleule, naamini ni muhimu mno kuhakikisha tunaweka utaratibu wa kisera na kisheria wa kulinda bidhaa zetu za ndan. Bado nasisitiza kuwa Serikali iendelee na juhudi za kuhakikisha kuwa tunaongeza uzalishaji wa mafuta ya kula nchini,” alisema.

Amesema amekuwa akihimiza viwanda vilivyopo nchini kulindwa na njia nzuri zaidi ya kutekeleza hilo, hususan kwa viwanda vya mafuta ya kula, ni kuzuia uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. “Uzuiaji huu utasisimua uzalishaji wa ndani wa mafuta ya kula, hasa mafuta ya mawese na alizeti,” amesema.

“Kasi ya kulinda viwanda vyetu hivi, inapaswa iwe kubwa na ya haraka sana, bado kuna maeneo yamefichika sana, tukiyakalia kimya kwa sasa madhara yake kwa nchi ni makubwa. Mfano mzuri ni bidhaa ya betri. Kuna smuggling (uingizaji wa bila kulipa kodi/magendo) kubwa ya betri kutoka nje na kuathiri kabisa hata mauzo ya ndani ya viwanda vya betri vilivyopo nchini,” amesema Zitto.

Amegusia kiwanda cha betri cha Panasonic alichosema kimeathiriwa mno na uingizwaji wa betri kutoka nchi za Asia wakati betri hizo hazilipiwi kodi hivyo bei yake kuwa ndogo kuliko betri zinazozalishwa nchini.

Mwenendo huo umesababisha kiwanda cha Panasonic kuwa hatarini kufungwa, hatua itakayolazimu Watanzania wanaofanya kazi hapo kukosa ajira, bali pia na serikali itakosa mapato ya kodi yaliyokuwa yakipatikana kutokana na kiwanda hicho kuzalisha.

“Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya China, mwaka 2016 jumla ya betri zenye thamani ya Dola milioni 36.5 (zaidi ya Sh. milioni 81) zililetwa Tanzania. Lakini kwa upande wa Tanzania, takwimu za TRA na TBS zinaonesha Tanzania iliagiza betri za thamani ya Dola milioni 5.3 tu (wastani wa Sh. bilioni 11) kutoka China,” amesema.

Zitto amesema mtindo huo unamaana kwamba zaidi ya asilimia 80 ya betri zinazoingizwa kutoka nchini China haziingizi kodi. Kwa upande mwingine, ina maana serikali inaruhusu bidhaa za ndani ya nchi kunyimwa fursa ya ushindani wa haki na bidhaa zinazotoka nje ambazo hazilipiwi kodi.

“Jambo hili lina athari kubwa sana kwa Taifa, hasa kwenye mapato ya kodi yanayopotea. Lakini wanaoathirika zaidi ni wazalishaji wa ndani wa betri. Maana bei za bidhaa za magendo ni pungufu zaidi, na hivyo huleta ushindani zaidi kwenye soko,” amesema Zitto ambaye amehimiza ujenzi wa viwanda vipya kwa vile vilivyojengwa zamani haviendesheki mpaka kwanza mifumo yake ya uzalishaji ibadilishwe kutokana na teknnolojia ya sasa.

Dr Slaa afunguka haya kuhusu ujio wake Tanzania!!!

Image result for dr slaa
Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Willbroad Slaa amesema hana mpango wa kurudi Tanzania kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa hazina ukweli wowote.

Slaa alijiuzulu ukatibu mkuu wa CHADEMA na siasa za vyama baada ya CDM kumpokea Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa urais 2015

BUNGE LA TANZANIA LAPOKEA UGENI MZITO HUKO BUNGENI DODOMA!!!

unnamedSpika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya Mhe. Alojz Peterle (kulia) pale ugeni wa Wabunge kutoka Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.ASpika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.A 1Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza  jambo pale alipopata ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.A 4Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wanne kulia) akipiga picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Mhe. David Martin (wanne kushoto) baada ya kumalizika kikao kilichofanyika  leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.A 3Wageni wa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ambao ni Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakifwatilia Vikao vya Bunge vinavyoendelea leo Mjini Dodoma.

Msanii Linah Sanga afunguka haya kuhusu ujauzito wake!!!

Image result for linah sanga
Linah Sanga 'Ndege Mnana' amefunguka na kuweka wazi kwamba haoni tatizo yeye kupiga picha za kuachia tumbo lake lenye ujauzito wazi kwani picha ni za kawaida sana wala hazina matatizo yoyote. Linah amefunguka hayo kwenye kamera za eNewz na kudai kwamba hawezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wake huku akidai wakosoaji wapo wengi.

PROF Jay atema cheche bungeni kuhusu vilio vya wasanii.

Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii kama makarai ya kujengea.

Prof Jay alisema hayo  Bungeni wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2017/ 2018 

"Wasanii wa Tanzania wamekuwa katika mazingira magumu sana na wamekuwa katika umasikini mkubwa licha ya mara nyingi kutumiwa katika kampeni mbambali na hata katika chaguzi zilizopita mmeona jinsi wasanii walivyokuwa wakitumika, mmewatumia kama makarai na baada ya hapo mmeyaweka uvunguni, tunajua makarai huwa yanatumika kwenye kujenga maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikikamilika yanawekwa uvunguni hayatakiwa kuonekana hata kwa wageni" alisema Prof Jay 

Mbali na hilo Prof Jay amesema wasanii wengi wa Tanzania wanakuwa masikini sana sababu wakishatumika huwa hawathaminiwa tena na kuachwa mpaka wakati mwingine wa uchaguzi au kampeni 

Mange kimambi amtolea povu zito POLEPOLE!!!

Baada ya Pole pole kuandika hiyo post hapo juu ikiwa imemtaja Mange Kimambi, Mange akaamua kumtolea  uvivu kama ifuatavyo :
.
#Regrann from #mangekimambi_ - :

"PolePole Tokea uwe katibu uenezi wa CCM ile brain ya kuongea mapoint mazito mazito imetoweka kabisa Yani. Hivi PolePole unakumbuka ulivyokuwaga unawa-inspire watanzania kwa jinsi ulivyokuwaga unaongea mapoint mazitoooooo. Siku hizi unaongea kama Bashite. Huna point, unajibu vitu bila busara, unajibu mambo kiwepesi wepesi...
.
.
Hivi Kweli Polepole kweli kati ya yote niliyosema point kubwaaaaa uliyoiona wewe ni Mimi kusema Kinana ameacha kufanya kazi za Chama???? And it's 100% true kinana amegoma kufanya mambo ya chama mpaka Baba Bashite A.k.a mwenyekiti wa CCM akamueleze why alimuitia TISS. Kinana alishikiliwa Na TISS nyumbani kwake for over 2 weeks...
.
Kwa issue ya Kinana alivyokaaa vibaya kwa Sasa ilibidi nyinyi kama chama muwatoe hofu wana CCM Na watz kwa ujumla kwa kuweka wazi data kuwa siku ile Rais anasema kamtuma kinana india kwa matibabu Ni kweli alikuwa india mtaje na hospitali aliyokuwa amelazwa, aliondoka TZ tarehe ngapi kwa ndege gani Na alirudi lini after that itakuwa easy watu kuhakiki habari hizo..
.
.
Polepole naomba uongeeee hadharani kuwa Kinana hakuita mkutano na waandishi siku ile Na kwamba Hakuzuiliwa Na TISS nyumbani kwake na kwamba hakutolewa silaha na Tiss. Na kwamba hakuwahi kuwa under house arrest chini ya TISS.Hiyo ndo response Watanzania wanayoitaka Na sio unatoa Majibu mepesi mepesi yasiyo Na point like je nikokuonyesha picha za kinana akifabya kazi za chama utanipa nini? Yani umejibu ka mtoto wa miaka mitano. That's a shallow answer to such a deep issue? Tena kutoka kwa mtu uliekuwaga unachambua mambo kwa kina, ukituonyesha picha za zamani ukasema ni za recent tutajua vipi? Ndo maana nakwambia umetoa majibu shallow. Na kama alifanya lazma kulikuwa na media tuonyeshe link tukaangalie sio picha zako wewe za kuchomoa chini ya godoro, tunataka picha zilizokuwa released Na media. Ukinionyesha hizo ntakupa hii account iwe account ya CCM.
.
.
Kama wewe kweli unajiamini jibu mambo ya TISS. Najua you can't do that sababu ni ukweli Na unaogopa siku Kinana au Nape wakiamua kufunguka utaaibika so huwezi shubutu kusema Tiss hawajawahi kumzuia kinana..CCM jibuni issue ya TISS kumshikilia Kinana, sio mnakuja namajibu ya KiBashite." Mange Kimambi

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 7 MAY ,2017



Maswali magumu yenye majibu magumu kutoka kwa Lipumba haya hapa!!!

 
Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ana mgogoro na chama chake cha CUF, jana alitinga studio za Clouds TV kujibu mapigo ya hasimu wake, Maalim Seif Sharif Hamad katika kipindi cha 360 na mambo matatu yalijitokeza.
Alichukua hatua hiyo baada ya kipindi hicho cha 360 kumuhoji Maalim Seif juzi na kumsukumia lawama Profesa Lipumba kuwa ndiye anayesababisha mgogoro katika chama hicho, akisaidiwa na Serikali.
File:Ibrahim Lipumba.jpgMaalim Seif, ambaye alimtuhumu Lipumba kuwa msaliti, alisema ni bora kukaa meza moja na CCM kuliko mwanasiasa huyo msomi wa uchumi kwa kuwa chama hicho tawala kinajulikana kuwa adui wa CUF hivyo ni rahisi kuchukua tahadhari.
CUF ipo katika mgogoro baada ya Profesa Lipumba kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake Agosti 2015 kwa kile alichoeleza kuwa nafsi inamsuta na mwaka mmoja baadaye aliandika barua ya kubatilisha uamuzi huo.
Hata hivyo Mkutano Mkuu wa CUF, uliofanyika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, haukukubali Profesa Lipumba kurejea madarakani, badala yake ukakubaliana na barua yake ya kujivua nyadhifa zote, hali iliyoanzisha mgogoro na viongozi wenzake.
Katika mahojiano hayo ya jana, Profesa Lipumba alizungumza na kujibu mambo mbalimbali lakini kati ya hayo, masuala matatu yalikuwa na utata zaidi.
Jambo la kwanza ni pale Profesa Lipumba alipoulizwa na watangazaji wa kipindi hicho sababu za kwenda kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CUF uliofanyika Agosti 21, 2016 wakati hakuwa mjumbe.
Lipumba alijibu kuwa aliitwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo ambao alisema walimtumia ujumbe mfupi wa simu na baadhi kumpigia simu.
“Nilipigiwa simu na wajumbe 12 wakiniambia ‘hapa kwenye mkutano mkuu, barua yako (ya kujiuzulu) inasomwa. Sisi wajumbe tunataka uje uthibitishe hii barua ndiyo yenyewe uliyoandika?” alisema Lipumba.
“Nilipata simu kama kumi au kumi na mbili. Nikaamua kwenda kwenye eneo la Mkutano Mkuu.Niliondoka nyumbani mimi na dereva mpaka kwenye Mkutano Mkuu.”
Maelezo hayo yalimfanya mtangazaji aulize sababu za kwenda kwenye Mkutano Mkuu wakati hajaalikwa na si mjumbe wa mkutano huo.
“Ah! Mimi nimeitwa na wajumbe kwamba hapa unahitajika kuja kuthibitisha,” alisema na kupandishiwa swali jingine.
“Hiyo imekaaje kikanuni. Unapotakiwa kuja kuthibitisha, kikanuni imekaaje. Unaalikwa kwa kutumiwa barua?” aliulizwa.
“Hapana nilitumiwa ujumbe wa simu. Katika taratibu zetu sisi ujumbe wa simu, barua ni utaratibu halali kumualika mtu kuhudhuria kikao,” alisema.
“Sasa sikujua nani ana-chair (mwenyekiti) nani katibu wa kikao kile, lakini nimekwenda kwenye mkutano mkuu. Nimefika eneo la mkutano nimekuta vijana, walinzi wa chama, blue guard, Nimeshuka wamenipokea, wakaniingiza ndani ya ukumbi wa Mkutano Mkuu. Wakanipeleka mahali nikaenda kukaa.”
Alisema alikuta mjadala kuhusu aitwe kujieleza, lakini mwenyekiti (Julius Mtatiro) alikataa na baada ya mapumziko, walipiga kura na kutangaza matokeo kuwa waliokuwa wanamtaka Lipumba ni wajumbe 14 na waliomkataa ni 476.
“Hiki ndicho chanzo cha sokomoko kutokea na kusababisha wajumbe kuimba ‘ni heri ya Jecha (Salim Jecha) aliyefuta matokeo kuliko Maalim Seif kutangaza matokeo wakati kura hazikupigwa’,” alisema Profesa Lipumba.
Jecha ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Mahojiano hayo pia yalijikita katika sababu za uamuzi wa Lipumba kujiuzulu.
Katika mahojiano hayo, Lipumba alisema aliamua kujiuzulu kwa sababu aliona si sahihi kwa Edward Lowassa kuingia ndani ya Ukawa na kugombea urais na kwamba hakuwa kinara wa kumshawishi Lowassa kujiunga upinzani.
“Ni uongo na mimi nilipata taarifa kutoka kwa (mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James) Mbatia kuwa Lowassa anahitaji kuzungumza na mimi na hata siku moja sikuwahi kuomba niunganishwe naye,” alisema.
Aliongeza kuwa hata siku moja hakuwahi kuomba namba ya Lowassa.
Alipotafutwa jana, Mbatia alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kuhusu kinachoendelea ndani ya CUF.
Juzi, Maalim Seif alisema ana ushahidi kuwa Profesa Lipumba alikwenda kumtafuta Lowassa ajiunge na Ukawa na alimuomba Mbatia amuunganishe naye.
Wakati akimkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa Julai 2015, Profesa Lipumba alisema suala la ufisadi ni mfumo na si la mtu mmoja mmoja.
“Sisi tunaponda ufisadi na mfumo wa kifisadi na chanzo kikubwa cha ufisadi ni mfumo ndani ya CCM, kwanza tuing’oe CCM, hapo ndipo tutakapoweza kuondoa ufisadi,” alisema Lipumba wakati wa kumtambulisha Lowassa wakati huo.
“Lowassa alikumbwa na tuhuma za ufisadi mwaka 2008, leo ni 2015 lakini ufisadi umeongezeka au umepungua? Lowassa hayupo serikalini? Tatizo ni mfumo na jambo la kwanza ni kuing’oa CCM.”
Lakini jana, Lipumba alisema kuwa hakusema Lowassa ndiye awe kamanda wa kuongoza vita dhidi ya ufisadi.
Hata hivyo, katika mahojiano hayo Profesa Lipumba alikiri kwenda nyumbani kwa Lowassa na kufanya mazungumzo kuhusu watu wanaomuunga mkono kujiunga na Ukawa.
Alieleza kuwa mipango yote ilisukwa na Chadema na kitendo cha yeye kuhusishwa katika mchakato wa kumshawishi Lowassa ulikuwa ni propaganda.
Alisema hatua yake ya kumlaumu Maalim Seif imetokana na katibu huyo mkuu huyo kufanya vikao na Chadema bila kumshirikisha yeye.
Kuhusu nguvu yake ndani ya CUF, Profesa Lipumba alisema baadhi ya wanachama walimfuata kumshawishi ashiriki kampeni kwa kuwa walimtambua kama bado mwenyekiti.
“Walikuja kina mbunge wa Temeke, Abdallah) Mtolea na (mbunge wa Kinondoni, Maulid) Mtulia kuniomba nishiriki kampeni zao, nikawaeleza siwezi kutokana na hali ilivyo kwa kuwa nitaharibu uhusiano kati yao na Chadema,” alisema
Akizungumzia suala hilo jana, Mtolea alithibitisha kuwa alienda kwa Lipumba kumuomba ahudhurie uzinduzi wa kampeni kama mwanachama wa kawaida.
“Nilimuomba akanikatila kwa sababu ya Lowassa. Nikamweleza mkutano ni wangu mimi siyo wa Lowassa akakataa pia,” alisema Mtolea.
Kuhusu kuwa msaliti, Lipumba alisema “waliosaliti ni wale waliofanya utaratibu wa kumleta Lowassa”.
Sababu za kujiuzulu,
Akizungumzia sababu za kujizulu, Profesa Lipumba alisema ni ukosefu wa umoja ndani ya CUF, hasa baada ya Ukawa kuundwa.
Alisema wakati mwingine, vikao vilifanyika bila yeye kupewa taarifa. “Nikajikuta nina wakati mgumu kulinda maslahi ya umoja na maslahi ya chama na ukosefu huu ulitumiwa na Chadema kuwadhalilisha wagombea wa CUF Bara,” alisema.
Alisema Chadema walisema CUF haina fedha za kusimamisha mgombea na taarifa hizo walipewa na Maalim Seif.
Kuingia ofisini
Profesa Lipumba alisema baada ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa kumtambua kama Mwenyekiti alikwenda moja kwa moja hadi ofisi ya makao ya chama hicho, Buguruni na kukanusha kuwa hakuvamia.
Alisema anamtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu, lakini alishangaa kwa nini hafiki ofisini.
Alisema tayari ameshamwandikia barua ya kuitisha kikao cha kamati tendaji kisha Baraza Kuu la Uongozi.
Aliongeza kuwa hakuanza kutofautiana na Maalim Seif baada ya kujiuzulu bali wakati wa mchakato wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya.
Alisema Maalim Seif alitaka muungano wa mkataba wakati msimamo wa chama ilikuwa ni Serikali tatu.
CUF ina wabunge 42, na kati ya hao ni wawili tu wanaomuunga mkono Profesa Lipumba

Mzee Mkapa asema haya kuhusu serikali ya Magufuli na sakata la vyeti feki!!!

Image result for mkapa
Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa mara ya kwanza amezungumzia utawala wa Rais Dkt John Pombe Magufuli huku akimpongeza utendaji kazi wake unavyokwenda.

Rais Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

Mzee Mkapa aliyesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumzia ni utawala wa Rais Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, masuala ya uchumi.

Alisema Mkapa kuwa, wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa madarakani bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 3,2017

KESI YA MADAWA YA WEMA SEPETU YAFIKIA HAPA MAHAKAMANI!!!

Image result for WEMA SEPETU
Malkia wa filamu , Wema Sepetu, Jumanne hii amepanda tena katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam, kusikiliza kesi ya tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya, ambapo upande wa Jamhuri umekamilisha upelelezi wa kesi inayomkabili msanii huyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ameahirisha kesi hiyo mpaka June 1, mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza maelezo ya awali ya upelelezi huo.

Muigizaji huyo, ambaye yupo nje kwa dhamana baada kusota mahabusu kwa siku 7, anadaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake, kufuatia msako mkali wa kupambana na dawa za kulevya uliofanywa na ofisi ya mkoa wa Dar es salaam.

ZITTO AFUNGUKA HAYA MAZITO KUHUSU MDEE!!!

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa shukrani kwa Bunge la Tanzania kwa kumsamehe Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa kuendelea na vikao vya Bunge.

Mbunge Zitto ametumia ukurasa wake wa Facebook kutoa shukrani hizo kwa bunge. Ameandika hivi:

 Hatimaye Waziri Kivuli wa Fedha ndg. Halima Mdee amesamehewa na ataendelea na vikao vya Bunge. Hii ndio haki. Mtu aliomba radhi hadharani, kwanini aadhibiwe. Shukran Kwa Bunge.

Halima Mdee alituhumiwa kutumia lugha chafu bungeni wakati wa uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki, Aprili 14 mwaka huu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 29



 

Total Pageviews