MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuwa ikiwatesa na kuwasumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.
Lema alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunafahamu jitihada za serikali ya awamu hii ya kupigania sera ya viwanda ambalo ni jambo jema.
“Kila mwenye akili timamu analipongeza ili suala la viwanda liwe na ukweli ni lazima wawekezaji na wafanyabiashara wawe na mazingira bora.
“TRA wamekuwa wakitesa na kusumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya hasa katika mkoa ninakotoka, TRA wanatumia polisi, Takukuru na usalama wa taifa kuwatishia katika masuala ya kodi.
“Ili waweze kufanya biashara zao kwa uhakika nini kauli ya serikali juu ya mfumo wa TRA?”alihoji Lema.
Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema ni kweli kipo chombo kinachowajibika kukusanya kodi kutoka kwa walipa kodi wakiwamo wafanyabishara.
“Ni kweli wanatambau ulipaji kodi ni wadaiwa sugu, TRA kupitia chombo chake Task Force makao makuu, ilikuwa na mkakati wa kuwapitia wadaiwa sugu. polisi, Takukuru walienda kule kuona hakuna utoaji rushwa.
“Na katika msafara huo kama Arusha, polisi walikuwa wanatumia silaha na utaratibu kama fedha zinaweza kulipwa papo kwa papo na nimshukuru RC wa Arusha kwa kuwaita wafanyabishara na kuwaeleza wale polisi walikuwapo kwa ajili ya kulinda tu na alirudisha amani.
“TRA inao utaratibu, wale ambao wanadhani haiwatendei haki kusikiliza kero watumie madawati hayo kupeleka malalamiko hayo.
“Serikali inawaheshimu wafanyabishara na inatambua umuhimu wao wa kulipa kodi na kila mmoja atambue wajibu wetu na waendelee kutoa ushirikiano na haiwapelekei hofu,”alisema Majaliwa.
0 comments:
POST A COMMENT