Rais John Magufuli amemteua Profesa Raphael Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana imeeleza kuwa uteuzi wa Profesa Chibunda unaanza jana tarehe 24 Aprili, 2017.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Chibunda alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sayansi na Teknolojia katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia.
Profesa Raphael Chibunda anachukua nafasi ya Profesa Gerald Monela ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amewasili mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
0 comments:
POST A COMMENT