Saratani ya matiti imekua ikiwatesa wanawake wengi kutokana na dalili zake kutoonekana mapema.
Pia wanawake wengi hawana tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na kupeleke kugundulika kuawana saratani ikiwa katika hali mbaya (late stage)
Kumbuka kujichunguza ndio njia bora ya kugundua saratani ikiwa bado ndogo, na una weza kujichunguza mara 2 au tatu kila mwezi.
Zifuatazo ni hatua tano muhimu katika kujichunguza kama una satratani ya matiti.
HATUA YA KWANZA
Simama mbele ya kioo mkono mmoja pembeni na angalia kama kuna mabadiliko yeyote kama vile uvimbe ,kovu,au matokwa yeyote kwenye chuchu.
HATUA YA PILI
Angalia kama kuna mabadiliko yeyote kwenye mistari ya kontua ya matiti.
HATUA YA TATU
Minya chuchu taratibu kama kuna uchafu wowote unaotoka
HATUA YA NNE
Lala kitandani kwa mgongo, weka mkono mmoja nyuma ya kichwa, papasa kwa kutumia mkono mwingine. Anza na papasa kwa mizunguko midogo midogo na uhisi
kama kuna uvimbe wowote ama maumivu.
HATUA YA TANO
Rudia hatua ya nne kwa upande mwingine wa titi.
Kama utaona dalili zozote usizo zielewa ni vyema kumuona daktari kwa vipimo na ushauri zaidi.
kumbuka kua kujichunguza mwenyewe sio mbadala wala haku zuii wewe kumuona daktari kwa ushauri na uchunguzi zaidi.
0 comments:
POST A COMMENT