UKISEMA Simba wamemficha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima,
utakuwa hujakosea kabisa kwani tangu kumalizika kwa mpambano wa watani
hao wa jadi hajaonekana tena uwanjani.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1,
Niyonzima ni moja ya wachezaji ambao walishindwa kuonyesha kiwango
kizuri na kuwafanya mashabiki kuondoka uwanjani vichwa chini.
Kiwango cha chini alichokionyesha Niyonzima katika mchezo huo
kilisababisha mashabiki wa Yanga kuanza kukumbushia miaka iliyopita
alipokuwa akihisishwa mapenzi yake ndani ya Simba.
Tangu mchezo huo dhidi ya Simba, Niyonzima hajaonekana tena na kikosi
cha Yanga kwenye mechi na Ruvu Shooting pamoja na ile ya juzi ya Mtibwa
Sugar, l
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa sababu kubwa ya kuondolewa Niyonzima katika kikosi cha Yanga ni mechi ya Simba.
Kwa sasa Mrwanda huyo aliyejiunga na Yanga Julai 2011 akitokea APR,
ameonekana kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Mzambia, George
Lwandamina, huku kukiwa na taarifa kuwa wapo kwenye mpango wa kumsajili
Kenny Ally kutoka Mbeya City ili awe mbadala wake.
Wakati mashabiki, viongozi na wanachama wa Yanga wakimwondoa kiungo wao
mchezeshaji kikosini kwa madai ya kuwa na mapenzi na Simba, daktari wa
kikosi cha Wanajangwani, Edward Bavu, amesema kuwa Niyonzima amekosekana
katika mechi hizo mbili kutokana na matatizo yakifamilia.
“Niyonzima hana tatizo la kiafya isipokuwa hakuweza kuwepo kwenye mechi
hizi mbili zilizopita kutokana na matatizo ya kifamilia ambapo uongozi
una taarifa hizo.
0 comments:
POST A COMMENT