Aubameyang ni mchezaji wa aina inayotakiwa na Liverpool - Steven Gerrard | HABARI ZA TOWN

~Jamvi La Habari Na Burudani~

Breaking News
Loading...

Aubameyang ni mchezaji wa aina inayotakiwa na Liverpool - Steven Gerrard


Kocha wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp yupo katika mbio za kutafuta mshambuliaji bora katika jitihada zake za kutegeneza kikosi bora kitakachowasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Mchezaji wa zamani wa Uingereza Steven Gerrard amesema Liverpool wanatakiwa kuvunja benki na kumsajili mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang mwisho wa msimu.

Jurgen Klopp yupo katika harakati za kutafuta mshambuliaji bora duniani katika jitihada zake za kutegeneza kikosi bora kitakachowasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Gerrard anaamini mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Aubameyang ndiye chagua sahihi linalo mfaa Klopp kama anataka kumalisha kikosi chake.

Alipoulizwa na mchambuzi mwenzake wa BT Sport, Gary Lineker kama Aubameyang ndiye mchezaji anayestahili kuichezea Liverpool, alijibu: “Yeah, kwa sababu aina yake ya uchezaji inazivutia klabu nyingi si Liverpool pekee.

Gerrard alisema Aubameyang ni mchezaji wa aina inayotakiwa na Liverpool.

“Ushambuliaji wake ni hatari kila wakati anapokuwa na mpira na jinsi anavyoweza kubadilika kwa haraka.”

Aubameyang ambaye kwa sasa ndio anaongoza kwa ufungaji katika Ligi ya Ujerumani baada ya kufunga mabao 21 katika michezo 21 alizocheza.
About Author
  • mwana habari Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Total Pageviews