Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka maofisa elimu wa shule za msingi na sekondari nchini, kuhakikisha vyama vya skauti vinakuwa na masomo ya ziada katika shule hizo.
Profesa Ndalichako aliyasema hayo hivi karibuni akiwa jijini Arusha kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya siku ya skauti Afrika ambayo kwa mwaka huu yalifanyika nchini.
“Kama rais wa skauti na waziri mwenye dhamana ya elimu, naomba nitoe wito kwa maofisa elimu wote wa mikoa kuhakikisha suala la skauti shuleni linakuwa ni sehemu ya masomo ya ziada. Nasema hivyo kwa sababu mikoa mingine hapa washiriki ni wachache na nauliza kwanini tunawanyima vijana kushiriki kwenye mambo ambayo yana manufaa kwa Taifa,” alisema.
“Tunataka wafanye nini, wakienda vijiweni hatuwaruhusu, hivyo tuwatengenezee mazingira na tutumie nguvu walizonazo katika mambo yatakayowajenga kuwa raia wema. Wakijiunga na skauti itawaongezea moyo wa kujitolea na kulipenda Taifa lao kwani kuna baadhi ya mikoa maofisa elimu hamjafanya kazi kikamilifu ndiyo maana klabu hazina nguvu,” alisema.
0 comments:
POST A COMMENT