Leo Machi 31, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amewasili nchini ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza mapokezi ya Waziri huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri Desalegn atakuwa nchini kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi, Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania, ambapo pia atasaini mikataba mitatu, Kutembelea bandari na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.
Ugeni huo utaipa Tanzania fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia kwa ugeni huo juu ya kukabili changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya kilimo cha kisasa katika maeneo yenye uoto wa asili wenye changamoto kama milima hapa nchini Tanzania.
0 comments:
POST A COMMENT