Msanii Diamond Platnumz anasema toka ameanza kufanya muziki ameweza
kufanya kazi na wasanii wengi lakini anadai ili akushirikishe kwenye
wimbo wake lazima umuonyeshe uwezo wako na sababu za kuitaka kolabo
yaje, hata kama upo chini ya uongozi wake haiwezi kuwa sababu yeye
kukupa shavu.Msanii Diamond Platnumz akiwa na RayVanny wakiwa kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' Diamond Platnumz alisema hayo kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kusema toka ameanza muziki wasanii ambao amewahi washirikishia kwenye nyimbo zake ni watatu, yupo Chid Benz, Maua, pamoja na RayVanny.
0 comments:
POST A COMMENT