
Msanii filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole amefunguka na kuweka
wazi kuwa yeye hana ujauzito wowote bali ameridhika na maisha jambo
ambalo limefanya aongezeke mwili na kunenepa licha ya watu kuwa na hisia
kuwa huenda ana ujauzito.
Shilole amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha 5SELEKT
kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi na
moja jioni mpaka saa kumi na mbili kamili.
"Mimi saizi sina ujauzito wowote sema nimenenepa tu maana nimeridhika na
maisha haya haya, ukimya wangu ni kwa sababu nilikuwa nazipa ngoma
nafasi saizi nimeamua kuja rasmi na wimbo wangu huu 'sitoi kiki' kwani
nimegundua Watanzania wanataka burudani, saizi pesa hakuna hivyo nimeona
bora nije kuwaliwaza na muziki mzuri huu" alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole amesema video ya wimbo huo ataifanya na waongozaji kutoka hapa hapa Tanzania.
0 comments:
POST A COMMENT