
Baadhi ya wagombea wa nafasi ya urais kupitia kwa chama cha wanasheria
wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama
wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa
kufanyika tarehe 18 ya mwezi huu.
Wamefikia hatua hiyo ili kuuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia
kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua
kesi katika mahakama kuu kupitia mkoa wa Dodoma na Dar es salaamu .
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mgombea TUNDU
LISSU amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi
huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuuharibu
uchaguzi huo
Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona
uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho kusisitiza
kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango
mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.
Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na
wanachama hao, washtakiwa ni mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na
chama chenyewe (TLS).
Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa
waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa LAWRENCE MASHA amebainisha kuwa
chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea
nafasi ya uongozi katika chama hicho huku akiwataka wanachama wa chama
hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao
unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha siku ya tarehe 18 ya mwezi huu
0 comments:
POST A COMMENT