DAR ES SALAAM: Taarifa mbaya ya kusikitisha kutoka kwa staa wa nyimbo za Injili, Rose Muhando zinadai kuwa, mwimbaji huyo anasakwa na uongozi wa Sober House ya Pederef ili waweze kumwokoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’.
Chanzo kilicho karibu na mwanamama huyo ambaye amejijengea jina kubwa kupitia nyimbo zake nzuri kama Nibebe, kimeeleza kuwa Rose ametoweka nyumbani kwake mjini Dodoma baada ya kutopea kwenye matumizi ambapo kuna kiongozi mmoja wa dini ameamua kumsaidia.
“Kuna kiongozi mmoja wa dini hapa Dodoma, ameamua kujitolea kumsaidia Rose baada ya kusikia hali yake ni mbaya. Ameamua kuwatafuta Pederef ili wamsake popote alipo na wakimpata wampeleke soba moja kwa moja na gharama zote yeye atazishughulikia,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya Rose ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipopatikana alioomba aachwe kwani alikuwa kanisani, angempigia mwandishi baadaye.
“Nitakupigia baadaye, nipo kanisani…,” alisikika Rose na kukata simu. Hata alipopigiwa tena baadaye, simu yake haikupokelewa.
Hata hivyo, Wikienda ilimtafuta mmliki wa Sober ya Pederef, Nuru Saleh aliyekiri kupewa kazi ya kumtafuta Rose na kumfikisha katika soba yao iliyopo Dodoma na kuanza kumpatia tiba ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
“Ni kweli. Sisi ndiyo kazi yetu. Nimepewa hiyo kazi na kiongozi wa dini, naomba nisimtaje lakini tumeshaanza kumtafuta na tukimpata tu, tutampeleka kwenye soba yetu ya Dodoma,” alisema Nuru.
Mara kadhaa Rose amewahi kuripotiwa kuwa anabwia unga lakini mwenyewe amekuwa akikanusha.
0 comments:
POST A COMMENT