
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kelele
zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya
dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la
Twendezetu Kigamboni lililofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam ambako
alisisitiza kwamba mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni vita vya ya
kufa au kupona.
“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele na mwangwi
unaoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema
Makonda.
Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma
kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee
kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.
“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na
maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si
rahisi,” alisema Makonda.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na vingozi wengine wa serikali akiwemo
Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile, Katibu Tawala wa Wilaya
hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
0 comments:
POST A COMMENT