
Kuwa superstar sometimes ni raha sana… why? Ukiwa kama Jay Z na Beyonce
unakuwa na uwezo wa kununua kitu chochote kile upendacho ikiwemo nyumba
ya bei ghali kuliko zote jijini Los Angeles nchini Marekani!
leo jumanne ya March 7 2017 imenipeleka moja kwa moja mamtoni ambapo
mtandao wa PEOPLE umeripoti kuwa weekend iliyopita The Carters walikuwa
jijini Los Angeles wakitafuta nyumba ya kuanzia maisha mapya na kuvutiwa
zaidi na nyumba ya bei kubwa kuliko zote jijini humo.
Nyumba hiyo yenye ukubwa wa mraba 57,000 inapatikana maeneo ya Holmby
Hills ambapo awali ilikuwa inamilikiwa na Television Producer Aaron
Speeling na mke wake Candy toka mwaka 1991. Baada ya kufariki kwa Aaron
Spelling mwaka 2006 ambaye ndiye aliyeijenga nyumba hiyo, mkewe aliamua
kuiweka nyumba hiyo sokoni kwa bei ya $150 Million lakini kufikia
October mwaka 2016 nyumba hiyo ilikuwa inauzwa kwa bei ya $200 Million.
Ndani ya nyumba hiyo, kuna vitu mbalimbali ikiwemo maktaba ya kusomea,
chumba kikubwa cha sinema, gym ya mazoezi, chumba cha midoli, studio ya
kucheza mchezo wa bowling, hifadhi kubwa ya wine, vyumba vya kulala
visivyo pungua sita, jiko sita, na bafu 26 . Mbali na vile
vinavyopatikana ndani ya nyumba hiyo, nje ya nyumba hiyo kuna uwanja
zaidi ya mmoja wa tennis, bustani yenye ukubwa wa ekari 5 pamoja na
swimming pool.
Sources karibu na The Carters wanadai kuwa familia hiyo inataka kuhamia
jijini LA moja kwa moja na wangependa kuimiliki nyumba hiyo haraka
iwezekanavyo.
0 comments:
POST A COMMENT