
Mama ya watoto hao anayeisha pwani ya magharibi Marekani anamimba kubwa na inasemekana atajifungua hivi karibuni.
Nyota huyo wa Real Madrid (32), aliwaambia watu wake wa karibu kuwa
mapacha hao watafikia katika jumba lake kubwa lililojengwa kwa gharama
ya pauni 5 milioni katika jiji la Madrid.
Chanzo hicho kilisema: “Cristiano na familia wake wamejianda kuwapokea watoto hao katika familia yao.
“Nyota huyo hataki kuweka wazi maisha yake binafsi, lakini aliwaambia
rafiki zake wa karibu kuwa anategemea kupata watoto wa kiume hivi
karibuni.”
Ronaldo kwa sasa anamahusiano na mrembo Georgina Rodriguez (23), haijawahi kusemwa kwamba anategemea kupata watoto mapacha.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kuficha jina la mwanamke aliyezaanaye
kama ilivyokuwa kwa mama wa mtoto wake Cristiano Jr, inasemekana
mwanamke huyo alipewa pauni 10 milioni na Mreno huyo kutojitangaza kuwa
ni mzazi mwezie.
0 comments:
POST A COMMENT