Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Dkt.
Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za kiutendaji
zinazomkabili ikiwemo uendeshaji wa shirika hiloAkitoa taarifa kwa waandishi wa habari Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amesema moja ya tuhuma zinazomkabili ni pamoja na kuingia mikataba kiholela.
Shirika la Elimu Kibaha ni Shirika la umma linalotoa huduma mbalimbali likiwa na ofisi zake Mkoa wa Pwani kilomita 40 Magharibi mwa Mji wa Dar es salaam.
0 comments:
POST A COMMENT