
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewajibu wote wanaosema
katika mitandao ya kijamii, kuwa mkewe si raia halali wa Tanzania na
kusema kuwa, hata kila siku wataamka na kisa kipya yeye bado ataendelea
kupambana na kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi.
Makonda ameyasema hayo alipokuwa ibadani katika kanisa la kiinjili la
kilutheli KKKT Ushirikia wa Kimara ambapo alisema baada ya kuona
wameshindwa kwa tuhuma hizi sasa wanaibua tuhuma zingine.
Aidha Makonda alisema kuwa anamfahamu historia ya vita dhidi ya madawa
ya kulevya ya kuwa hakuna mtu aliyetoka salama. Wote walioanzisha
mapambano haya hawakutona salama, wengi waliuwawa, wengine walifungwa na
wengine walipata matatizo mbalimbali sababu wahusika wa biashara hii ni
watu wenye nguvu.
0 comments:
POST A COMMENT