Kazi ya kuchunguza majina 97 yaliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na
Dawa za Kulevya, imeanza kufanyiwa kazi kwa vigogo watano waliotajwa
kuhojiwa.
Februari 13, Makonda alimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers
Sianga orodha ya majina 97 ikiwa ni awamu ya tatu ya watuhumiwa wa
biashara ya dawa za kulevya.
Kamishna wa Intelijensia wa Mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema jana
kuwa wanawahoji na wanafanya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao kabla ya
kuwafikisha mahakamani.
“Tuna watu muhimu watano wanaotoka katika orodha ile ya mkuu wa mkoa.
Tunao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na muda ukifika tutawatajia
mtawafahamu,” alisema Kamishna Kibula na kuongeza:
“Hatukamati ovyoovyo ni lazima tujiridhishe bila shaka kwamba wahusika
wana sifa ya kukamatwa. Pia hatutangazi ingawa tunafanya operesheni za
kiuchunguzi ambazo zinafanyika mara kwa mara.”
0 comments:
POST A COMMENT