
Juzi hivi nilipata kumsikiliza Mh Paul Makonda akielezea historia ya
maisha yake iliyojaa changamoto nyingi. Clip hiyo ikanikumbusha maneno
aliyoniambia Paul Makonda mwaka 2009 wakati tunakwenda Dodoma.
Alivyoeleza kwenye clip ndivyo alivyonisimulia siku ile tukiwa safarini
kwenda Dodoma. Siku ile alipokuwa akinisimulia aliishia kulia kwa
uchungu. Pia niliumia sana.
Alipokuwa akinisimulia, mara kwa mara Paul Makonda alisema "lakini
sikukata tamaa niliendelea kumtumaini Mungu". Hakukata tamaa na ndiyo
sababu ya yeye kufika alipofika.
Kuna picha inaonyeshwa na kudaiwa hapo ndipo alipozaliwa. Sehemu duni.
Kuna picha zinaonyeshwa Paul akiwa kwenye mazingira duni, kuna picha
zinamwonyesha akilia, lengo ni kumdhalilisha.
Rejeeni historia za watu maarufu duniani leo, wengi walikuwa watu wa
kawaida na huenda duni lakini walikabiliana na changamoto bila kukata
tamaa na wakashinda. Mmoja ni Baraka Obama.
Obama kwao ni Kenya. Na alipokuwa anagombea mara ya kwanza republicans
walitoa picha ya Obama akiwa na bibi yake kijijini kwenye nyumba duni,
lengo wamdhalilishe. Obama hakukata tamaa na hatimae akawa rais wa
Marekani ambayo yalikuwa makusudi ya Mungu.
Hakuna binaadam amayepanga azaliwe wapi na wazazi wapi. Watu wengi, kwa
kukabiliana na changamoto katika maisha hufanikiwa kubadili maisha yao
na kufikia mafanikio makubwa, hasa kwa kutokata tamaa na kumtumaini
Mungu. Vijana nilidhani mngejifunza hilo kwa Paul Makonda badala ya
kukejeli.
Kingine ambacho nimeona nikiandike, mimi ukweli nashangaa kuona wengi
wanaomdhihaki Paul Makonda siyo wapagani. Ni watu wenye dini, tena dini
maarufu. Inasikitisha sana.
Kuwa na dini na kumjua Mungu ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuwa
kiongozi wa dini lakini humjui Mungu wa Kweli. Tabia moja kuu ya Mungu
ni upendo. Mungu ni pendo. Pendo huvumilia, hustahimili, nk. Hivyo,
tabia hii inatakiwa kudhihirika kwa watumishi wa Mungu.
Yesu Kristo alimfunua au alidhihiridha upendo wa Mungu alipokuwa
msalabani akiteseka ili aukomboe ulimwengu. Akiwa msalabani alisamehe,
hakulaani. Alipnyesha upendo wa Mungu. Alipotukana na kudhihakiwa
hakurudidha mashambulizi bali alibariki. Aliposingiziwa, hakuwatisha
waliomsingizia bali aliwaombea. Yesu Kristo alitoa pepo na kuyaelekeza
apepo yaende kwa nguruwe, hakuyapeleka kwa binaadamu aliokuja kuwaokoa.
Lakini hali inavyoonekana sasa inasikitisha. Hilo nalo tujifunze.
Vijana wengi wanaangamia kwa kutumia madawa ya kulevya. Bila hatua
madhubuti kuchukiliwa, ninahofu inawezekana Tanzania ikatawaliwa tena.
Tena kirahisi tu. Hapatakuwa na rasilimali watu wenye kuwajibika na
kulilinda Taifa hili.
Paul Makonda kathubutu, vijana na watanzania kwa ujumla, tuache itikadi
ya vyama vya siasa tuunge mkono juhudi za kupiga vita madawa ya kulevya
kwani madawa ya kulevya yanalingamiza taifa.
0 comments:
POST A COMMENT