Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa
ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na
fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya
kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa
kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama
ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi,
jeshi na kwenye michezo.
Mifano mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino
Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander
McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs
(Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine.
Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.
Japokuwa mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika
kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao
wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini
mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama
nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.
Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi
kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa
wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa
kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.
Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo
wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama
wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji,
utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.
Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga
waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia
wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee
ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili
(heterosexual world).
0 comments:
POST A COMMENT