
Rapa ambaye amejizolea umaarufu sana kupitia mitandao ya kijamii
Harmorapa amefunguka na kusema kwa Tanzania hii hajaona msanii wa
kumfananisha na Alikiba na kusema hata ngoma yake ambayo amefanya na
Juma Nature alitaka kufanya na Alikiba.
Harmorapa anasema kabla ya kurekodi ngoma yake hii mpya ambayo amefanya
na mkongwa Juma Nature alijitahidi sana kumtafuta Alikiba ili aweze
kufanya naye lakini jitihada zake ziligonga mwamba kutokana na ukweli
kwamba Alikiba alikuwa na mambo mengi na kushindwa kumfikia kuzungumza
naye jambo hilo.
"Kiukweli King Kiba kwa Tanzania hapa sioni wa kumfananisha naye, kwa
hiyo nisema sijaona bado wa kumlinganisha naye sababu jamaa anafanya
vizuri sana na anajua muziki sana, hata kabla ya kurekodi hii kazi yangu
mpya nilifanya jitihada na watu wa karibu na Alikiba japo niweze
kufanya naye kazi lakini sikuweza kufanikiwa kutokana na mambo yake kuwa
mengi sana na watu pia ambao walikuwa wakinipa connection naye kuna
vitu sikuweka sawa, na muda nikaona unazidi kwenda nikasema ngoja
nifanye tu" alisema Harmorapa
0 comments:
POST A COMMENT