Producer kutoka kiwanda bora cha muziki cha muda wote Bongo Record laber P Funk Majani amesema ni mapema sana kwa sasa kumtafuta au kumpata malkia wa muziki wa Hip hop hapa bongo kama ilivyo kwa wanaume
Majani amekiambia kipindi cha The Playlist kuwa kuna wanawake wengi wanafanya vizuri lakini wanahitaji ushindani zaida ili waweze kupata mmoja mkali kuliko wote kama ilivyo kwa Fid Q ambaye hana ushindani kwa sasa kwenye muziki wa Hip Hop hapa nchini
“Kwa sasa ni mapema sana kumtafuta mkali wa Hip Hop kwa wanawake hapa bongo maana, ukicheki kama @rosa_ree anastyle tofauti na ladha ya kivyake, @chemical_tz anandika vizuri stori japo wote ni wakali na wanafanya kitu kizuri nadhani tuwape muda wapate ushindani ili apatikane mkali”
0 comments:
POST A COMMENT