
ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anajivunia uamuzi wake wa
kutojihusisha na siasa maana amepata amani ya moyo kuliko wasanii
wenzake ambao kwa sasa wapo kwenye malumbano ya kisiasa.
Mrembo huyo ambaye ni mkali wa sinema za Kibongo, alisema, wakati wa
Kampeni za Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015, watu wengi walikuwa walikuwa
hawamuelewi lakini ukweli ni kwamba aliliona hili ambalo linatokea kwa
sasa ambapo wasanii wanaumbuana, wanasemana na kuwagawa mashabiki.
“Unajua watu wengi walikuwa hawanielewi kwa nini sipendi siasa na
ninajua wazi wengi waliniona labda mimi naringa sitaki kujumuika na
wezangu lakini siyo hivyo nilijua nini kinaweza kutokea mbeleni kama
ilivyo sasa,” alisema Lulu kufafanua anazungumzia malumbano yapi hasa.
Hivi karibuni, Muigizaji Wema Sepetu alitangaza kujitoa CCM na kujiunga
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo alitupa dongo kwa
CCM kwa kusema anawadai hela za kampeni hali ambayo iliwaibua wasanii
wenzake, kumpinga vikali kwa maelezo kuwa walilipwa.
0 comments:
POST A COMMENT