
Baada ya kujiunga Vevo Diamond February 26 ameyaandika yafuatayo >>>”Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo vevo… nikawambia uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida”
“Vevo
wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond
toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama
tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji
wa video hiyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo”
“Mbali
tu ya kumlipa, VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia
kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na
ukubwa na nafasi yake atokapo” hivyo
nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya,
vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu
ya Youtube kawaida.
SABABU YA KUYASEMA HAYA:
Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu.
Vilevile
umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichukua juu ya sanaa zetu
kwa sasa maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae…
nafahamu Wasanii wengi hawakuwa wakilifahamu hilo na badala yake kuingia
@VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu.
kwa
uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio
umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine
nimekosea Tafadhali mnisameh…
-SIMBA #MALENGO“
0 comments:
POST A COMMENT